dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, June 26, 2017

MWINYI ATAMANI MAGUFULI AWE RAIS WA MAISHA!!!

Mwinyi: Utawala wa Rais Magufuli ulipaswa kuendelea kuwepo miaka yote

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema kama si utawala wa katiba uliopo nchini, utawala wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwepo miaka yote.

Mwinyi ameyasema hayo leo (Jumatatu) wakati akitoa salam za Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Amesema anayoyafanya Rais Magufuli ni mambo mazuri na kwamba kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kulipeleka taifa mahali kuzuri.

"Amelipeleka taifa mahali kuzuri, amerudisha nidhamu, sasa hivi ukienda hospitali unapata huduma vizuri, ukienda kwenye ofisi unapata huduma nzuri," amesema. "Yako mengi mazuri, tumuunge mkono Rais wetu, kama isingekuwa katiba basi ningesema aendelee kuongoza mpaka mwisho," ameongeza.

No comments :

Post a Comment