dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, June 28, 2017

Taarifa kuhusu utata wa Biashara ya Gesi Tanzania na Kenya!

Taarifa iliyotumwa kwa umma kutoka Wizara ya Biashara na Uwekezaji inasema kwamba Tanzania itaendelea kuheshimiwa kwenye mikataba ya Kibishara na Nchi Kenya.
Tarehe 24 Aprili, 2017 magazeti nchini Kenya yalitoa taarifa ya kwamba Serikali ya Kenya itapiga marufuku uingizwaji wa gesi ya kupikia (
Liquefied Petrolium Gas, LPG ) nchini humo kutokea Tanzania, na kwamba gesi itakayoruhusiwa kuingia Kenya ni ile itakayokuwa imepitia kwenye Bandari ya Mombasa peke yake. Baada ya kusoma taarifa hizi Serikali ya Tanzania iliwasiliana na Serikali ya Kenya ili kupata maelezo kuhusu hatua hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibiashara katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Tarehe 18 Mei, 2017 Serikali ya Kenya ilitekeleza uamuzi wake kwa kuzuia shehena ya gesi isiingie Kenya kutokea Tanzania. Hatua hii ina athari kubwa kwa wafanyabiashara wa gesi ya kupikia hapa nchini pamoja na watu wote ambao ajira zao zinategemea biashara hii. Wakati hatua hizi zinachukuliwa bado Serikali ya Kenya ilikuwa haijatoa maelezo rasmi kwa Tanzania kuhusu uamuzi wake huo. Katika kikao cha Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kilichofanyika tarehe 2 Juni, 2017, suala la hatua ya Kenya kupiga marufuku uingizwaji wa gesi kutokea Tanzania lilizungumzwa kwa kirefu na kufanyiwa maamuzi. Kimsingi Serikali ya Kenya ilikubali kuondoa katazo la uingizaji wa gesi kupitia Tanzania mara moja, na makubaliano haya yaliingizwa kwenye kumbukumbu za Mkutano ambazo ziliafikiwa na nchi zote wanachama wa Jumuiya kwa kuweka sahihi. Pamoja na makubaliano haya, Kenya imeendelea kuzuia gesi isiingie nchini mwao kutokea Tanzania. Serikali ya Tanzania imewasilisha rasmi malalamiko yake Kenya kuhusu suala hili



No comments :

Post a Comment