dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, June 29, 2017

Trump Rasmi aanza vita na Waislam!

Rais wa Marekani, Donald Trump ameweka masharti mapya ya maombi ya hati za kusafiria kwa mataifa sita ya Kiislamu na wakimbizi duniani.

Moja ya masharti hayo ni kuwa anayeomba visa lazima awe na uhusiano na mtu mwenye ushirikiano wa kibiashara na Marekani.

Nchi zinazoguswa na masharti hayo ni pamoja na Iran, Libya, Somalia, Sudan Syria na Yemen.

Ujumbe kuhusu masharti hayo umetumwa katika balozi zote za nchi hizo.

Masharti hayo mapya yameanza kutekelezwa jana na yanagusa pia mahusiano ya kifamilia kama mzazi, mkeo ama mumeo, mtoto wa kiume ama wa kike aliye Marekani.

Masharti hayo yanatolewa baada ya Mahakama Kuu nchini Marekani kusitisha  kwa muda agizo la Rais Trump  la kuzuia nchi za Kiislamu kuingia Marekani, zuio ambalo lilikosolewa.

No comments :

Post a Comment