dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 30, 2017

Fatma karume amshtaki polisi aliyemzogoa mahakamani, adai fidia bil. 1!

WAKILI wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam.

Katika kesi hiyo, Fatma anahitaji alipwe na Inspekta Mwampondela Sh bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake, kumbugudhi na kumzuia kufanya kazi yake (assault, battery, misfeasance in public office).

Fatma amesema Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu hali iliyomsababishia maumivu kwenye mkono wake.“Aliniambia kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani ili amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa shikwa mwili wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho kwa wengine,” amesema Fatma.

Fatma ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja wake ili aweze kupata dhamana.

/ MTANZANIA

No comments :

Post a Comment