dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, July 14, 2017

LOWASSA ARIPOTI POLISI, ATAKIWA KURUDI TENA ALHAMISI IJAYO!

Baada ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuwasili katika ofisi ya mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, kama alivyotakiwa kufanya Juni 29, ameruhusiwa kuondoka na kutakiwa kurudi tena Alhamisi ijayo.

 Mwanasheria wa Lowassa, Peter Kibatala amezungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa Lowassa ametakiwa kurudi Alhamisi bila sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo kuwekwa wazi.

“Hatujaambiwa kwa nini ila tumeambiwa tuje alhamisi ijayo kwa ajili ya maelekezo na kuwasikiliza zaidi,” alisema.

Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa kwenda katika ofisi za DCI ambako anahojiwa kwa tuhuma za uchochezi.

 Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alihojiwa Juni 28 na Juni 29 na Wakili Kibatala alizungumza na wanahabari mara baada ya mahojiano hayo.

Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya kichochezi Juni 23, mwaka huu katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

No comments :

Post a Comment