dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 27, 2017

Maalim Seif Amvaa Spika wa Bunge Job Ndugai!

Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba hatua ya Spika kuwavua ubunge , udiwani na kuteua wengine wapya  inalenga kudhoofisha kambi ya wabunge wa  CUF na Ukawa.

Amesema Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge kujiridhisha kwanza.

 Spika Job Ndugai anadhani Watanzania ni vichaa wamuamini kuwa alishachukua hatua ya kujiridhisha kuwa wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefukuzwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Ndani ya siku moja?”amehoji Maalim.
Amesema Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama?

Amesema yeye kama katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25  akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu.

“Angekuwa na nia ya kweli ya kutaka kujiridhisha si hapo ndipo pangekuwa pa kuanzia kwa kuwepo kile wanasheria wanachokiita shaka inayoweza kuingia akilini yaani ‘reasonable doubt’?’’ amehoji.

Amesema  Spika Ndugai aliyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania. Hapo ndipo Spika Job Ndugai alipolifikisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments :

Post a Comment