dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, July 29, 2017

Polisi yamdaka Kigogo wa Acacia uwanja wa ndege, Dar!

Taarifa ambayo Nipashe iliipata kutoka kwenye vyanzo vyake jana na baadaye kuthibitishwa na Acacia kupitia tovuti yao, ilieleza kuwa kigogo huyo alikumbana na mkasa wa kukamatwa na kisha kutupwa selo wakati akiwa Airport kujiandaa kwenda nje ya nchi.

“Ukamataji wenyewe ulifanyika kitaalamu sana…ni kwa mbinu za hali ya juu kama zile za filamu za kininja,” chanzo hicho cha uhakika kiliiambia Nipashe bila ya kueleza kwa kina juu ya muda wa ukamataji huo na kuongeza:

“Huyo kigogo alifika Airport na kuwa mbioni kusafiri. Ghafla askari wakamtokea na kumdaka juu kwa juu na kuondoka naye.”Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, alisema yuko safarini hivyo jambo hilo waulizwe watu wa Dar es Salaam.

Aidha, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, aliiambia Nipashe kuwa suala hilo aulizwe msemaji wa kikosi cha jeshi hilo kwenye viwanja vya ndege ambaye hata hivyo, hadi gazeti hili likienda mitamboni, mwandishi hakufanikiwa kumpata msemaji huyo.

Aidha, jana, Acacia kupitia tovuti yao, walituma taarifa iliyokiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa aliyekamatwa Airport wakati akiwa mbioni kusafiri ni Meneja Mkuu wa mgodi wa Buzwagi.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mkuu huyo alikamatwa wakati alipofika uwanjani hapo na hati yake ya kusafiria ilishikiliwa kwa muda.

Aidha, taarifa ilieleza kuwa baada ya kukamatwa, uongozi wa Acacia ulifanya taratibu za kisheria na baadaye kufanikisha kuachiliwa kwake pamoja na kurejeshewa hati yake ya kusafiria.

“Acacia tunafanya kazi na washauri wetu wa masuala ya kisheria na mamlaka husika kwa ajili ya kusaidia wafanyakazi wetu dhidi ya masuala kama haya,”sehemu ya taarifa hiyo ya Acacia ilieleza.

Pia ilieleza kuwa kampuni hiyo inathibitisha kwamba inafanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria zote za Tanzania na wamekuwa wakitangaza kila kitu kuhusu thamani halisi ya wanachozalisha na wamekuwa wakilipa kodi sahihi na mirabaha.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Acacia itaendelea kutoa taarifa sahihi kwa wateja wake mara kwa mara kuhusu masuala yanayotokea Tanzania, majadiliano na mambo ambayo yatakuwa yameibuliwa kuhusu kampuni yao.

Hivi karibuni, serikali ilizuia usafirishaji wa mchanga wa madini (makinikia) kwenda ughaibuni baada ya kamati mbili teule za wataalamu zilizoundwa na Rais kuchunguza makontena 277 yaliyozuiwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kubaini kuwapo kwa tofauti kubwa ya taarifa zilizokuwa zikitolewa na kiwango halisi cha madini yaliyokuwa yakisafirishwa.

Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iliitaka kampuni ya Barrick ambayo inamiliki hisa nyingi za Acacia kulipa kodi ya dola za Marekani bilioni 190, sawa na zaidi ya Sh. trilioni 400.

TRA ilisema kuwa kodi hiyo ni matokeo ya taarifa zisizokuwa sahihi kuhusiana na madini yaliyochimbwa kuanzia mwaka 2000.

Aidha, jana kulikuwa na taarifa zilizothibitishwa na Acacia kuhusiana na ujio wa maofisa wa Barrick nchini wiki ijayo kwa nia ya kuendelea mazungumzo na serikali katika kufikia muafaka wa mgogoro uliojitokeza.

Akiwa katika ziara zake za kikazi mkoani Kigoma, Rais John Magufuli aliwataka Barrick kuharakisha mazungumzo baina yao na serikali kuhusiana na kulipa kiasi kikubwa cha fedha wanachodaiwa na nchi.

Pia alionya kuwa iwapo wangechelewa, serikali haitasita kutaifisha migodi yao na kuikabidhi kwa Watanzania ili mwishowe ipate kodi yake.


/ Nipashe

No comments :

Post a Comment