dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, July 29, 2017

RAIS AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI!

 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea wakati wa kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala 
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea wakati wa kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitoa maagizo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt.  Anna Peter Makakala baada ya kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiendela kutoa maagizo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala na Makamishna wa Idara hiyo baada ya kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala na Makamishna wa Idara hiyo baada ya kikao chake na Makamishna wa uhamiaji makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala. Picha na habari na Ofisi ya Waziri Mkuu.

RAIS Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo asimamishwe kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.
Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.
Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”
Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini jambo hilo kwa kina: “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu...Sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia.”
Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.
"Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali. Hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."
Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. " Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."
Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.

No comments :

Post a Comment