dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, July 7, 2017

Serikali Uganda imesema hakuna kufuga kucha, kuvaa kimini na kujipodoa!

Kama ulikuwa una ndoto za kufanya kazi nchini Uganda hasa kwa watoto wa kike wenye kupenda kujipodoa na kuvaa nguo zinazoonyesha maumbile basi jua hautaweza kudumu wala kupata kazi nchini humo.

Hii ni kutokana na sheria mpya iliyopo, Kwa mujibu wa mtandao wa edaily wa Kenya, umeripoti kuwa serikali ya Uganda imepiga marufuku uvaaji wa nguo fupi makazini, upakaji make up uliozidi, kubandika kucha ndefu na bandia, kuweka nywele bandia na kuzipaka rangi, kuvaa nguo inayobana kama vile Tshirt na magauni pamoja na kuvaa vivalio.

Miaka 2013 nchi hiyo ilitunga sheria ya kukataza kuvaa nguo fupi, sheria ambayo ilizua mijadala nchini humo na sehemu zingine.

No comments :

Post a Comment