dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 18, 2017

Hali ya siasa Zanzibar kujadiliwa kesho!


Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, inatarajiwa kufanya kikao kesho Septemba 18 mwaka huu kujadili hali ya kisiasa Zanzibar, chini ya Makamu  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu,  imesema kikao hicho cha siku moja kitafanyika katika Ukumbi wa ofisi kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Taarifa hiyo imesema luwa pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitapokea na kujadili kwa kina taarifa ya hali ya kisiasa ya Zanzibar pamoja na taarifa nyingine mbali mbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, vile vile kikao hicho kitapokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika ngazi za Wilaya kwa kipindi cha 2017-2022, kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Imeelezwa kuwa kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC - Zanzibar kilichofanyika Septemba 16, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”, kwa ajili ya kuandaa Ajenda za kikao hicho.

No comments :

Post a Comment