dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 17, 2017

Afrika Kusini: Rais Zuma afanya mabadiliko katika baraza la mawaziri kwa mara nyingine!

Kwa mara nyingine rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefanya mabadiliko katika baraza la amwaziri Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa habari,waziri wa elimu na katibu jenerali wa chama cha SACP Blade Nzimande amevuliwa wadhfa wake.

Blade Nzimande alikuwa mmoja ya waliokuwa wanamtaka rais Zuma ajiuzulu.

Waziri wa mambo ya ndani Hlengiwe Mkhize ndie ameteuliwa kuchukua nafasi ya kiongozi huyo wa SACP.

Kumekuwa na mabadiliko kadha wa kadha katika baraza hilo ikiwa ni mara ya pili kwa rais Zuma kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri mwaka huu.

Mnamo mwezi Machi,Rais Zuma alimvua madaraka waziri wa fedha Pravin Gordhan,hali iliyosababisha uchumi wa Afrika Kusini kushuka kwa asilimia kubwa.

No comments :

Post a Comment