dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, January 18, 2018

Picha ya Selfie kwenye Facebook yasababisha muuaji kupatikana Canada!


Mkanda unaovaliwa na Cheyenne Antoine (kushoto) unaonekana kwenye picha na rafiki yake Brittney Gargol.
Mwanamme mmoja nchini Canada amepatikana na hatia ya kumuua rafiki yake baada ya polisi kugundua kuwa kifaa kilichotumiwa kuua kilichokuwa kwenye picha ya kujipiga (selfie) ya wawili hao iliyokuwa katika mtandao ya kijamiii.

Cheyenne Rose Antoine, 21, alikiri siku ya Jumatatu kumuua Brittney Gargol, 18, Machi mwaka 2015.

Gargol alipatikana amenyongwa karibu na Saskatoon, Saskatchewan, huku mkanda wa Antoine ukiwa kando na mwili wake.

Antoine alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa mauaji

Alitajwa kama mshukiwa baada ya kuchapisha picha ya selfie kwenye mtandao wa Facebook, ikionyesha amevaa mkanda uliotumika saa kadhaa kabla ya Gargol kuuliwa.

Alisema walikuwa wamekunywa pombe na pia wakavuta bangi kabla kuanza kuzozana.

Polisi wanasema kuwa taarifa ambayo alikuwa amewapa, kuwa Gargol aliondoka na mwanamume mmoja huku naye akionda kumuona shangazi yake.

Ndipo wakatumia picha zake za Facebook kufuatilia mienendo ya wawili hao usiku huo.

No comments :

Post a Comment