dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, May 16, 2018

Vigogo 60 kitanzini upotevu wa mabilioni!

UCHUNGUZI na ukaguzi maalum uliofanyika kwenye vyama vya ushirika nchini umewaweka matatani vigogo 57 wa vyama hivyo kutokana na kubainika kuhusika katika vitendo vya ubadhirifu wa takribani Sh. bilioni sita.Kutokana na kubaini kasoro hiyo wakati wa ukaguzi, serikali kupitia Wizara ya Kilimo imechukua hatua mbalimbali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuondoa bodi za uongozi na watendaji wa vyama hivyo.

Pia imewahoji viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kutokana na tuhuma za ubadhirifu zinazowakabili.

Viongozi waliohojiwa ni pamoja na vyama vya ushirika vya Muhimbili Saccos, Mlimani Saccos, BoT Saccos, Mbinga Saccos, Kurugenzi Mbinga Saccos, Ayalabe Saccos, Madibila Saccos, Wazalendo Saccos na Arusha Kurugenzi Saccos.

Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, ndiye aliyetoa taarifa hiyo jana bungeni alipowasilisha hotuba ya makadiri ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.

Alisema tayari hati za madai zimeandaliwa kwa watuhumiwa 57 wa ubadhirifu wa Sh. bilioni 5.95 katika vyama saba.

"Watuhumiwa wanne wa ubadhirifu katika chama cha Wazalendo wamefikishwa mahakamani na rufani zilizokatwa na watuhumiwa wengine sita, hati za madai zinashughulikiwa,” Dk. Tizeba alisema na kuongeza:

"Katika kuimarisha usimamizi wa Saccos, wizara imeingia makubaliano na Taasisi ya Dun and Bradstreet Credit Bureau Tanzania Ltd ya kutengeneza mfumo wa kieletroniki wa usimamizi (Saccos Supervision Software) ambapo kwa sasa upo kwenye majaribio.”

Waziri huyo alisema mfumo huo utawezesha kupatikana taarifa za mara kwa mara juu ya maendeleo ya Saccos pamoja na kufanya usimamizi kwa ufanisi na urahisi zaidi.

Vilevile, Dk. Tizeba alisema wizara yake imefanya ukaguzi maalum katika vyama nane vya ushirika visivyo vya kifedha vya Matendo AMCOS, Luponde AMCOS, Mbifacu AMCOS Ltd, Lupembe AMCOS Ltd, Sudi AMCOS, Lihimalyao AMCOS, Rivacu Ltd na Mamcu Ltd.

"Matokeo ya uchunguzi huo yalibaini uwapo wa ubadhirifu na ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 kwenye vyama vya Mbifacu Ltd na Mamcu Ltd uliosababishwa na usimamizi na utendaji mbovu wa viongozi na watendaji," alisema.

Aliongeza kuwa watuhumiwa wamefikishwa kwenye mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.

Tangu kuingia madarakani Novemba 5, 2015, serikali ya awamu ya tano imekuwa ikisisitiza kupambana na wabadhirifu kwenye mashirika na taasisi za umma.

Katika kutilia mkazo mapambano hayo, tayari imeshaanzisha divisheni maalum ya makosa ya ufisadi na uhujumu uchumu kwenye Mahakama Kuu, maarufu Mahakama ya Mafisadi.

No comments :

Post a Comment