dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, June 18, 2018

ACT wafanya uchambuzi wa Bajeti ya seriakali!


Chama cha ACT Wazalendo kimesema bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha, 2018/19 inawaumiza wafanyakazi na wakulima nchini.

Maoni hayo yametolewa jana, Juni 17, kwenye mkutano wa kuchambua bajeti hiyo baina ya chama hicho, wahariri, waandishi wa habari na wadau wengine wa uchumi na biashara.

Akiwasilisha uchambuzi wa chama hicho, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema utekelezaji wa bajeti hiyo utapungua kwa asilimia 23 huku wafanyakazi na wakulima wakiendelea kuumia.
"Kuna wastaafu 7,000 wa miaka miwili iliyopita ambao hawajalipwa mafao yao mpaka leo. Wengine 3,000 wanatarajiwa kustaafu Julai Mosi bila malipo hayo," alisema Zitto.

Kuwapa unafuu, amependekeza kodi ya mshahara (PAYE) ipunguzwe na michango kwenye mifuko ya jamii ifanyiwe marekebisho.

Chama hicho kimependekeza kushushwa kwa michango ya pesheni kutoka asilimia 20 mpaka 12 ili kuwapa unafuu wafanyakazi na waajiri.

"Kama ilivyo kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi nao walipe asilimia tano huku waajiri wao wakichangia asilimia saba," alisema.

Kwenye kilimo, alisema bajeti yake imepunguzwa kwa asilimia 23 licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi huku kikiajiri asilimia 66 ya Watanzania wote.

Chama hicho kimeishauri Serikali kuzipa kipaumbele sekta zinazogusa maisha ya wananchi wengi kwa kukamilisha miradi na mipango inayoanzisha.

"Serikali imepanga kuanzisha akaunti jumuifu ya Hazina itakayotunza fedha za bodi za mazao. Suala hili litapunguza utendaji wa baadhi ya taasisi hasa bodi hizo," alisema Zitto.

Alisema fedha za wakulima wa korosho zimekatwa hivyo kuchelewesha salfa, dawa muhimu kwenye zao hilo hivyo akashauri maandalizi yafanyike zaidi kabla akaunti hiyo haijaanza kutumika.

No comments :

Post a Comment