THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY
|
TAARIFA KWA UMMA
USAJILI WA WATOA HUDUMA ZA MAUDHUI KWA NJIA YA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaukumbusha umma kuwa, usajili wa watoa huduma za maudhui
mtandaoni yaani wamiliki wote wa blogu, majukwaa mtandaoni (online forums), redio na televisheni
mtandaoni ulioanza rasmi tarehe 21 Aprili, 2018 unaendelea na hadi tarehe 10
Juni, 2018 jumla ya leseni 46 zimetolewa na jumla ya leseni 4 zimekamilika kwa
ajili ya kukabidhiwa rasmi kwa wahusika.
Kwa mujibu wa Kanuni 4 na ya 14 ya Kanuni za Maudhui
Mtandaoni za mwaka 2018 (The Electronic and Postal Communications
(Online Content) Regulations,
2018), watu wote wanaotoa huduma za blogu, majukwaa
mtandaoni (online forums), redio na
televisheni mtandaoni, wanatakiwa kujisajili TCRA na kupatiwa leseni ili kutoa huduma hizo. Jinsi ya kusajili tembelea tovuti
ya TCRA katika kiunganishi: www.tcra.go.tz,
kipengele cha ‘Online Contents Application System'. Kwa ufafanuzi au maelezo zaidi
tumia barua pepe: onlinecontent@tcra.go.tz
Pamoja na jukumu la kuelimisha Umma kuhusu Kanuni hizo
na kuwasajili watoa huduma, TCRA imepewa
pia jukumu la kuchukua hatua kunapotokea ukiukaji wa Kanuni za Maudhui
Mtandaoni za 2018, kwa lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwa na matumizi sahihi na
salama ya mitandao ya mawasiliano ya kielektroniki nchini.
Kwa hiyo, TCRA
inaendelea kuutahadharisha umma kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 18 ya Kanuni za
Maudhui Mtandaoni za 2018, ni kosa la kisheria kutoa huduma za maudhui
mtandaoni (blogu, majukwaa mtandaoni-online
forums, redio na televisheni mtandaoni) bila kuwa na leseni.
MAMBO YA KUZINGATIA:
1.0
Wale ambao wamekuwa wakitoa huduma za maudhui
mtandaoni na bado hawajapata leseni husika, wanatakiwa kujisajili kabla ya tarehe 15 Juni, 2018.
2.0
Kuanzia leo tarehe 11 Juni, 2018 hadi tarehe 15
Juni, 2018 hawaruhusiwi kuweka jambo/taarifa (post) yoyote zaidi ya zilizopo kwenye Blogu/Majukwaa/Redio
auTelevisheni mtandao zao leo na ambazo zinapitiwa pia.
3.0
Baada
ya tarehe 15 Juni, 2018 hatua za
kisheria zitaanza kuchukuliwa dhidi ya yeyote atakayekuwa anatoa huduma za
maudhui mtanadoni bila kusajiliwa na kupewa leseni kwa mujibu wa sheria.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
11 JUNI, 2018
No comments :
Post a Comment