Top Leaderboard Advert

Zacadia Patreon

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 2, 2018

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ltd) yafutarisha wateja wao Mkoani Mtwara!Sheikh Mkuu wa Mtwara Nurdin Mangochi akitowa Nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislam wakati wa futari maalum ilioandaliwa na PBZ Tawi la Mtwara kujumuika na Wateja wao iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Naf Apartment Mtwara.


Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakijumuika katika futari maalum ilioandaliwa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Mtwara wakifungulia na madafu baada ya kukamilika muda wa funga saa kumbi na mbili jioni hafla hiyo imefanyika katika Viwanja Hoteli ya Naf Apartment Mtwara. 
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa katika viwanja vya Hoteli ya Naf Mtwara wakijianda ya sala ya magharibi baada ya kufika wakti wa Sala na kuaza kupata futari ilioandaliwa PBZ Tawi la Mtwara. 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Alhajj Nurdin Mangochi akisoma dua baada ya kumaliza Sala ya Magharibi iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Naf Mtwara wakati wa hafla ya futari ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Limited, kwa ajili ya Wateja wao Mkoani Mtwara.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Alhajj Nurdin Mangochi akijumuika na Uongozi wa PBZ na Wananchi wa Mtwara katika futari maalum ilioandaliwa na PBZ Tawi la Mtwara iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Naf Apartment Mtwara. 
Wajumbe wa Bodi ya Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) wakijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara katika futari maalum ilioandaliwa na PBZ kwa Wateja wake Mkoani hapo iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Naf Apartment Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Juma Ameir Hafidh na Wajumbe wa Bodi ya PBZ wakijumuika na Wananchi wa Mtwara katika hafla ya futari maalum ilioandaliwa na PBZ Tawi la Mtwara kwa ajili ya wateja wao kujumuika na kubadilisha mawazo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hoteli ya Naf Apartment Mtwara. 
Wananchi wa Mtwara wakipata futari ilioandaliwa kwa ajili yao na Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Tawi la Mtwara katika viwanja vya Hoteli ya Naf Apartment. 
Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Chaguo la Watu wakijumuika na Wananchi wa Mtwara katika hafla ya futari iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Naf Apartment Mtwara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya Watu wa Zanzibar Bi. Kidawa H.Saleh akijumuika na Wananchi wa Mtwara katika futari ilioandaliwa na PBZ Tawi la Mtwara kwa ajili ya wateja wao iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Naf Apartments Mtwara.Mteja wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Sheikh Adam akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Mtwara wakati wa hafla hiyto ya futari iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Naf Apartments.na kutowa nasaha zake kwa Uongozi wa PBZ kuboresha zaidi huduma zao katika Mkoa wao ili kuweza kunufaika zaidi kupitia huduma mbalimbali za kifedha zinazotelewa na PBZ kwa Wananchi wa Mtwara. 

Wananchi wa Mkoani Mtwara wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya futari ilioandaliwa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Mtwara, katika viwanja vya hoteli ya Naf Apartments. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Bi. Kidawa H.Saleh akiwa na Wafanyakazi wa PBZ na Viongozi wakiitikia dua ikisomwa na Sheikh Mkuu wa Mtwara Alhajj Nurdini Mangochi akisoma baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari ilioandaliwa na PBZ Tawi la Mtwara, iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Naf Apartments.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Juma Ameir Hafidh, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Mtwara na Viongozi wa benki hiyo baada ya kumalizika hafla ya futari iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Naf Apartments Mtwara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Juma Ameir Hafidh, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Mtwara na Viongozi wa benki hiyo baada ya kumalizika hafla ya futari iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Naf Apartments Mtwara.

1 comment :

  1. eToro is the ultimate forex broker for newbie and pro traders.

    ReplyDelete