dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, June 7, 2018

Zitto azungumzia 'Ukawa' mpya itakavyokua!

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka kuwa Chama cha ACT Wazalendo Katika kikao chake cha Kamati Kuu cha Januari Mwaka 2018 kiliazimia kuwa ni muhimu kujenga mashirikiano na vyama vingine na makundi mengine ya kijamii.Akizungumzia ushirikiano huo wa kidemokrasia (DeFront), Zitto anasema hilo ni vuguvugu litakalohusisha si vyama vya siasa tu, bali makundi mbalimbali katika jamii.

Zitto amefunguka kuwa Chama cha ACT Wazalendo Katika kikao chake cha Kamati Kuu cha Januari Mwaka 2018 kiliazimia kuwa ni muhimu kujenga mashirikiano na vyama vingine na makundi mengine ya kijamii.

“Tunataka kujenga ‘The Democratic Front’ kwa kuhusisha wana Demokrasia nchini kwa madhumuni ya  kutetea, kuimarisha na kulinda demokrasia yetu ya vyama vingi pia kujenga Uchumi shirikishi wa Wananchi”, amesema Zitto

Zitto anafafanua kuwa tayari chama chake kimeanza mazungumzo na vyama vya siasa, asasi za kiraia na vyama vya wafanyakazi ili kufikia azma hiyo.

No comments :

Post a Comment