dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, July 6, 2018

NAPE NNAUYE : WATAPATA TABU SANA ...NDIYO SHIDA YA KUDANDIA TRENI KWA MBELE....



Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mh. Nape Nnauye amesema kwamba wanaomzushia kwamba amesimamishwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi watapata tabu sana.
Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya kusambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kwamba barua ya Mbunge huyo kusimamishwa uanachama wa Chama chake imekwishamfikia mkononi.

"Kwa uzushi huu watapata tabu sana wanuka maziwa, ndio shida ya kudandia treni kwa mbele, unawakuta wenyeji unakuwa Mwenyeji kuliko" Nape Nnauye.

Aidha Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Nchi John Pombe Magufulia mapema wiki hii alionyeshwa kuchukizwa na wabunge wanaotokea mikoa ya Lindi na Mtwara kutokana na michango yao bungeni kwenye suala la korosho ambapo baadhi ya wabunge wa CCM kutokea mikoa hiyo waliitaka serikali iwalipe wakulima pesa ambazo wanadai ili waweze kuendeleza zao hilo.

Hivi karibuni Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo, Ado Shaibu alidai kwamba hakuna mwanaharakati anayeweza kulitetea Taifa akiwa chini ya Chama tawala hivyo kuwahimiza Nape, Bashe na Hawa Ghasia kuwa kama wana nia ya dhati ya kuwatetea wanyonge wahamie ACT-Wazalendo.

No comments :

Post a Comment