dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, July 7, 2018

Rais Magufuli kuwaongoza watanzania kupokea ndege Mpya KESHO Jumapili!



Dkt. John Magufuli kesho Jumapili Julai 08, 2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.

Hii ni ndege ya nne kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuimarisha huduma zake.

No comments :

Post a Comment