dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 10, 2018

JUKWAA LA WAHARIRI - TEF LALAANI MWANDISHI WA HABARI KUPIGWA NA POLISI!

Jukwaa la wahariri nchini limelaani vitendo vya kupigwa kwa waandishi wa habari vinavyofanywa na Jeshi la Polisi pindi wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Kauli hiyo imekuja kufuatia kupigwa kwa waandishi wawili siku ya Jumatano tarehe 8, Agosti ambapo mwandishi kutoka wilayani Tarime mkoani Sita Tuma aliyekuwa akitekeleza majukumu yake wakati jeshi hilo lilipowatanya kwa silaha za moto wafuasi wa CHADEMA waliokuwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Dodatus Balile amesema kuwa kitendo hicho cha kukamatwa kwa mwandishi na kushikiliwa wakati akiwa kazini si sahihi na taratibu za mamlaka haziruhusu vitendo dhidi ya wanahabari.

“Mwandishi amekamatwa akiwa kwenye eneo la kazi wala hakufika pale kwaajili ya kuandamana kama walivyodai wao, kama wao walivyokuwa kazini hata sisi tunakuwa kazini”, amesema Balile.

Tarehe 8, Agosti Jeshi la polisi , wilayani Tarime mkoani Mara, liliwashikilia Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko, mwandishi wa habari, pamoja na mara baada ya kuamuru wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), kusitisha kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea nchini.

No comments :

Post a Comment