Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 7, 2018

Ndoa ya Abdul Kiba mambo hadharani!


KAMA kama kama dawa, mama la mama nimedamshi ileile katika uwanja wangu wa kujidai. Nakuja kukupa ubuyu kama ilivyo desturi yangu. Ubuyu unanoga ukiwa ujachanganywa na vikorombwezo vya kutosha, ndio unapata radha tofauti kama ulivyo ubuyu wa leo wa mwanamuziki Abdul Kiba, ambaye alifunga ndoa na mkewe Rwahida, miezi michache iliyopita, imedaiwa ndoa hiyo tayari imeota mbawasasa hivi imeota mbawa na mkewe amerudi kwao upo?

Mtoa habari wetu wa kujitegemea amefunguka kuwa, Abdul Kiba mara nyingi amekuwa ni mtu wa kurudi nyumbani usiku na mara nyingi anashinda maskani maeneo ya Ilala Mtaa wa Arusha, kitu ambacho mkewe huyo amekiona kama sio sawa na pamoja na hayo bado anaona hakuna upendo ndani.
“Yaani Abdul kiukweli hana mapenzi kabisa na mkewe nafikiri alimuoa kwa shinikizo litakuwa la wazazi lakini sio mwanamke ambaye amempenda kutoka moyoni kwa sababu mara nyingi mwanamuziki huyo unamkuta Ilala mpaka saa nane usiku ndio anaenda kwake na wala hana muda wa kuongea na mkewe huyo,” alisema mleta ubuyu huyo.

Baada ya gazeti hili kupata ubuyu huo, lilimtafuta Abdul ambaye ambapo alipopatikana alimuomba mwandishi wetu azungumze na meneja wake aitwaye Rehema.

Ijumaa Wikienda likaona isiwe kesi, likamtafuta Rehema ambapo alifunga kama ifuatavyo:

Wikienda: Mzima dada? Kuna habari imetufikia kuwa ndoa ya Abdul na mkewe imevunjika hivyo ungeweza kutupa ukweli kwenye hilo kwa maana mwenyewe kasema tuzungumze na wewe.

Rehema: Hizo habari hata sisi tumezisikia kwamba watu wanasema hivyo lakini naomba kukuhakikishia hakuna ukweli wowote.

Wikienda: Sasa kwa nini watu wanasambaza uvumi huo?

Rehema: Unajua Abdul ni tofauti sana na Ally, yeye mara nyingi anapenda sana kuwa huru sana hivyo watu wakimuona pekee yake wanafikiria hivyo lakini sivyo au wengine wanasema kwa nini hamposti mkewe…

Wikienda: Kwa hiyo mke wake hajarudi nyumbani kwao?

Rehema: Tena kwa uhakika zaidi ongea na mkewe huyu hapa nipo naye hapa (akampa simu).

Wikienda: Enhe vipi dada kuhusiana na madai ya kuachana na mumeo?

Rwahida: Hakuna ukweli wowote mimi na mume wangu tupo vizuri tu kama kawaida hakuna kitu kama hicho.

Wikienda: Mh! Haya bwana asante.

Rwahida: Asante sana.

No comments :

Post a Comment