Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 10, 2018

Utulivu warejea baada ya mapigano makali ukanda wa Gaza!

Mpaka wa Gaza ulishuhudia utulivu hii leo baada ya makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliosimamiwa na Misri kumaliza vurugu zilizotikisa Kusini mwa Israel na ukanda wa Gaza kwa siku mbili.

Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano huenda yakakabiliwa na changamoto kubwa kufuatia wapalestina mjini Gaza kuamua kuanza tena maandamano yao ya kila wiki, ambayo mara kwa mara yanakumbwa na vurugu.Baada ya usiku mtulivu, jeshi la Israel liliwaambia wakaazi wake katika eneo la kusini waliokuwa katika maeneo ya kujikinga dhidi ya makombora kwamba kwa sasa wanaweza kurejea katika hali zao za kawaida.

Ongezeko la makombora yaliyovurumishwa mpakani mwa Israel na Gaza pamoja na mashambulizi ya angani katika wiki za hivi karibuni yamesababisha Umoja wa Mataifa na Misri kujaribu kufikia makubaliano kati ya pande hizo mbili hasimu ili kuzuwia mgogoro mkubwa zaidi.

Katika vurugu za siku mbili zilizopita mwanamke mmoja wa kipalestina aliyekuwa mja mzito, mwanawe wa miaka 18 pamoja na mwanamgambo mmoja wa Hamas waliuwawa huku watu takriban 7 wakijeruhiwa kutokana na maroketi yaliorushwa nchini Israel.

Hata hivyo maafisa wa Palestina wanasema makubaliano yamefikiwa kupitia mpatanishi ambaye ni Misri, lakini bado hapajakuwa na tamko rasmi kutoka upande wa Israel la kukubali kufikia makubaliano ya aina yoyote na kundi la Hamas. Kundi hilo la wanamgambo la Hamas linalotambuliwa na mataifa mengi ya Magharibi kama shirika la kigaidi tayari limepigana vita mara tatu na Israel ndani ya muongo mmoja uliopita.

No comments :

Post a Comment