Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 13, 2018

Dkt. Tizeba azungumza Bungeni kwa mara ya kwanza!

Dkt. Charles Tizeba
Aliyekuwa Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, leo amehudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma na kushangiliwa na Wabunge waliokuwamo Bungeni, pale Naibu Spika Tulia Ackson alipomtaja ili kuuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Dkt. Tizeba ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa, alisimama na kupigiwa makofi na wabunge wenzake, kisha akamuomba Naibu Spika kumruhusu kusema maneno mawili tu, na kusema kwamba …. “La kwanza ni kumshukuru sana Mh. Rais kwa Fursa aliyokuwa amenipa ya kulitumikia taifa, lakini pia nikushukuru wewe na Mheshimiwa Spika kwa ushirikiano nilioupata wakati nikitumika serikalini ndani ya Bunge lako”.Kauli hiyo iliendelea kupigiwa makofi na Wabunge wenzake, na kisha akauliza swali alilokusudia, ambalo lilihusu ujenzi wa vivuko vilivyomo kwenye jimbo lake la Buchosa.

Dkt. Tizeba alikuwa Waziri wa Kilimo ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Magufuli Novemba 10, 2018, kufuatia sakata la ununuzi wa korosho.

No comments :

Post a Comment