dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 13, 2018

Rihanna ampiga marufuku Rais Trump kutumia nyimbo zake!


Rihanna

Mwanamuziki Ri Ri ama mwite Rihanna amekuwa ni msanii wa hivi karibuni kuwa na uthubutu wa wa kutamka hadharani na kumtaka rais wa Marekani Donald Trump kuacha mara moja kutumia tungo zake katika mikutano yake ya kisiasa.

Mwanamuziki huyo ajulikanaye kama The Barbadian singer ametishia kuchukua hatua za kisheria baada ya wimbo wake wa mwaka 2008, unaokwenda kwa jina la Don't Stop the Music, kupigwa katika mkutano wa kisiasa wa raisi Trump huko katika maeneo ya Chattanooga.

Rihanna - ajulikanaye pia kama Fenty - timu yake imekwisha tuma barua rasmi katika Ikulu ya Marekani , White House, barua ambayo gazeti maarufu nchini humo Rolling Stone imeishuhudia.

Raisi Donald Trump akiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za katikati ya muhula
Na inasomeka hivi : "hili limetufikia raisi Trump amekuwa akitumia tungo za muziki za [Rihanna] na rekodi kuu,ikiwemo wimbo wake unaofanya vizuri wa Don't Stop the Music kuhusiana na matukio kadhaa ya kisiasa uliofanyika nchini Marekani.

"Kama wewe ni lazima au ujue, Bibi Fenty hakutoa idhini yake kwa Mheshimiwa Trump kutumia kazi zake ama muziki wake kutumiwa katika shughuli hizo. Kuendelea kwa matumizi hayo ni tabia isiyofaa.

Matumizi yasiyoidhinishwa ya matumizi ya tungo za mwanamuziki huyo kwenye mikutano ya raisi
Miongoni mwa wanamuziki waliothubutu kuzuia kazi zao kutumika katika mikutano ya kampeni za kisiasa , Rihanna anaungana na mamilioni ya wanamuziki hao nchini humo akiwemo Aretha Franklin alizuia wimbo wake wa Amazing Grace wimbo wenye mahadhi ya kidini na baadye ulitumika katika filamu moja baada ya miaka 46 .

No comments :

Post a Comment