dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 25, 2019

Korea Kaskazini yafyatua tena makombora ya masafa mafupi!

Korea Kaskazini imefyatua baharini kile kinachoonekana kuwa ni makombora mawili ya masafa mafupi katika pwani yake ya mashariki hii leo, ikiwa ni tukio la karibuni la mfululizo wa majaribio ya makombora katika wiki za karibuni.

Baraza la Usalama wa Taifa la Korea Kusini limesema kwenye taarifa yake kuwa Korea Kaskazini ilifyatua maroketi hayo kutokea jimbo la Hamgyong lililoko kaskazini mashariki mapema hii leo.

 Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza ni aina gani hasa ya maroketi yaliyofyatuliwa. Korea Kaskazini inafyatua maroketi hayo baada ya Marekani na Korea Kusini kumaliza luteka ya pamoja ya kijeshi mapema wiki hii.
Hapo jana waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Kaskazini alisema taifa hilo litajaribu kusalia kitisho kikubwa cha Marekani, iwapo itaendelea kuiwekea vikwazo.

Jaribio la leo ni la saba kufanywa na Korea Kaskazini tangu Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un walipokutana katika mpaka wa Korea hizo mbili mwezi Juni.

No comments :

Post a Comment