dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 12, 2012

Wanaolilia Muungano wa mkataba ni vibaraka

Na Mwinyi Sadallah
11th August 2012

Vigogo wachache wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wanaolilia Muungano wa mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar ni vibaraka wanaopigania kurejea kwa himaya ya Sultan Jamshid bin Abdullah aliyeangushwa na Chama cha Afro Shraz Party.

Kada maarufu wa CCM Zanzibar, Baraka Mohamed Shamte, alitoa matamshi hayo katika mahojiano maalum na NIPASHE nyumbani kwake Mkunazini mjini Unguja jana.

Shamte alisema kundi linalopigania juhudi hizo ameliita ni la vibaraka na wasaliti wapya waliolipwa ujira na fedha nyingi toka nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shamte alisema Waraabu toka Oman waliivamia Zanzibar na kuikalia kibabe kwa miaka 132 tokea mwaka 1832 hadi 1964 hadi pale chama cha ASP kilipofanya ukombozi wa haki kupitia njia ya Mapinduzi ya damu Januari 12, 1964.

Alisema jumla ya wafalme 11 waliikalia Zanzibar kwa zamu kinyume na matakwa ya waafrika waliokuwa wakikandamizwa kwa karne nyingi, wakionewa na wakibaguliwa katika nchi yao na kuyimwa haki za msingi bila ya kufanyika kura ya maoni.

“Utawala wa kifalme ulioitawala Zanzibar uliitisha mwaka gani kura ya maoni au kufunga mkataba na wanyeji wa kiafrika, waliivamia Zanzibar na kumuondoa kwa nguvu mtawala wa kienyeji enzi hizo aliyeitwa Mwinyimkuu na kuitawala Zanzibar bila ya ridhaa,“ alieleza Shamte.

Alisema wanaojitokeza sasa kutaka Tanganyika na Zanzibar ziwe na Muungano wa mkataba, aliwaita mawakala na vibaraka wanaopigania kuurudisha ukoloni huo kwa kigezo cha demokrasia ya vyama vingi na mjadala wa ukusanyaji na uratibu wa maoni ya Katiba mpya.

“Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walifunga mkataba uliokuwa na ridhaa kupitia vyama vyao, waliwauliza wananchi wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kuketi kwa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Bunge la Tanganyika,” alisema Shamte.

‘Namtaka Hassan Nassor Moyo na wenzake kwanza wawaonyesha waafrika wa Zanzibar mkataba uliofanywa kati ya Zanzibar na Sultan Oman kabla ya kutaka Muungano wa mkataba kati ya Zanzibar na Tanganyika.wakishindwa sitakosea kuwaita ni wasaliti wapya”. Alisema Shamte.

Kada huyo wa CCM alieleza kuwa Waoman walipewa ardhi baada ya mabeberu wa nchi za Ulaya kuigwa Afrika katika mkutano uliofanyika mjini Berlin huko Ujerumani mwaka 1884/1885 kinyume na hiari ya waafrika wenyewe wakiwemo Wazanzibari.

Shamte ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar Mohamed Shamte Hamad, alisema Waoman walipoivamia Zanzibar waliuangusha utawala wa kienyeji ulioongozwa na Mwinyimkuu ambaye alikuwa na Makao Makuu yake huko Dunga Mkoa Kusini Unguja.

Mwanasiasa huyo machachari alisema chama cha ASP kiliwachukulia waaarab toka Oman ni wavamizi waliojiingiza kwa nguvu na kuwakandamiza waafrika wa Zanzibar kwa miaka mingi kinyume na utu na heshima ya yao.

Alisema Uhuru kamili wa waafrika wa Zanzibar ni ule wa mwaka 1964 na siyo wa Disemba 10, 1963 kama inavyoaminiwa na vibaraka walioosalia Zanzibar wakienddelea kumuunga mkono Sultan aliyepinduliwa Zanzibar Januari 12,1964 Jamshed bin Abdullah.

Alitoboa siri na kutaja kuwa hata hati ya Uhuru wa mwaka 1963 hakupewa baba yake mzazi ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza na badala yake Mwakilishi wa Malkia wa Uingereza alimkabidhi Sultan Jamshid.

Alisema kitendo hicho peke yake kilionyesha ni jinsi gani hila na hadaa zilivyoandaliwa kati ya vyama vya ZNP , ZPPP, mfalme na Waingereza ili kuwalaghai waafrika.

Shamte ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa ASP Youth League, alisema ili kuthibitisha ZNP na ZPPP ni vyama vya Sultan, vilishindwa kupeperusha bendera yao na kujikuta wakipeperusha bendera ya rangi nyekundu iliokuwa na nembo ya karafuu chini ya utawala wa Oman.

Alisema chama cha ASP baada ya Mapinduzi, mara moja kilipeperusha bendera yake iliokuwa na rangi nyeusi, buluu ya maji bahari na kijani ili kuionyesha dunia kuwa chama cha waafrika wa Zanzibar kimeleta ukombozi wa haki na kuunda dola mpya.

CHANZO: NIPASHE


No comments :

Post a Comment