dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, June 20, 2013

Mikopo ya JK yatumika kuongeza wake Zanzibar

NA MWINYI SADALLAH

20th June 2013


Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Mfuko wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa kusaidia wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali umeshindwa kuleta tija Zanzibar, baada ya baadhi ya watu waliopata mikopo hiyo kutumia fedha hizo kuongeza wake.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Kazi, Uwezesheji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, wakati akijibu swali la Mwakilishi Saleh Nassor Juma wa Jimbo la Wawi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachofanyika Chukwani mjini hapa.

“Mfuko wa JK wa kusadia wafanyabiashara na wajasiliamali tija yake haikupatikana Zanzibar kama ilivyokusudiwa, wapo watu walionufaika na mikopo wametumia fedha kuongeza majiko (wake) na kufanya mambo mengine,” alisema Waziri Haroun.

Hata hivyo, alisema kwamba hali hiyo imechangiwa kwa kiwango kikubwa na kutolewa kwa fedha hizo kabla ya wahusika kupatiwa elimu ya kutosha kuhusu misingi ya biashara na maendeleo ya wajasiliamali visiwani humo.

Alisema kutokana na matatizo hayo, wizara yake imeamua fedha za mfuko huo kuchaganywa na mfuko wa maendeleo ulioanzishwa na Rais wa Zanzibar wenye lengo la kusaidia wajasiliamali na vikundi vya ushirika Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

1 comment :

  1. KUSEMA KWELI MIMI BINAFSI SIAMINI KUWA KIGENGE HICHI CHA VIBARAKA WA TANGANYIKA KAMA WAKO SIRIASI KATIKA UONGOZI WAO HAWA NI WAOGA,MAFISADI,WABAGUZI NA WABINAFSI SI WAKWELI NA WAMESHINDWA.TUNAONA MAMBO MENGI WANAYOYASEMA NA WANYOYATENDAAMBAYO YANAZIDI KUIRUDISHA NYUMA ZANZIBAR.KAMA HIYO MIKOPO KWA WAFANYA BIASHARA YOTE INAKWENDA KISONGE ,MAKUNDUCHI NA KWENYE MATAWI YA CCM SIO MIKOPO TU NI FURSA ZOTE KWA UJUMLA ILI KUIMARISHA CHAMA HALAFU BASI HAKUNA KINACHOFANYIKA NA WALOKOPESHWA HAWALIPI NA SERIKALI HAINA UBAVU WA KUWASHITAKI KWA SABABU HIZO NDIO KURA ZA CCM. KWA UONGOZI WENYE AKILI TIMAMU HIZO PESA ZA KIKWETE NA AMAANI NA HUYO SHUANI ZOTE KWA PAMOJA SI WANGEJENGA KITUO CHA KISASA CHA BIASHARA [CENTRO COMERCIALE]ILI KUWASAJILI HAO WAFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO NDANI YA HILO JENGO,HII INGESAIDIA SANA KATIKA UTEKELEZAJI,UKUSANYAJI WA KODI, BIASHARA ZA KIWANGO NA MAENDELEO YA KUDUMU LAKINI WAPI NIA ZENU SI NJEMA KWA ZANZIBAR MUNGU YUPO NA ANALIPA HAPAHAPA DUNIANI KILA MNAOLIFANYA HALIWI KWA UNAFIKI WENU DUA ZA WENYE KUDHULUMIWA ZINAFANYA KAZI NA TUTAANDAA HALBADIRI NYENGINE KWA AJILI YENU TU NYINYI MAFISADI TUMEKUCHOKENI HATUWATAKI KAZI YENU KUWAPUMBAZA HAO MASIKINI WA MUNGU WATU WA ZANZIBAR WANYONGE WATULIVU NA WASIKIVU .NIA MBAYA HAIJENGI.WANYONYAJI NA MAKABAILA WAKUBWA LAANA ZA ALLAH ZIWA JUU YENU.HAMNA LOLOTE POROJO TU.WAHARIBIFU WAKUBWA KISIWA CHA UNGUJA MSHAKIHARIBU CHOTE IMEKUWA KAMA JAA LA MAVI YENU SHENZI SANA HAWA WATU ROHO MBAYA NA VINYONGO KATIKA NAFSI ZAO UKIWAONA SURA ZAO ZINAELEZA KILA KITU.

    ReplyDelete