Balozi Seif azindua Hospitali ya jamii Mahonda
Kulia ya Balozi Seif
ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa,
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. Amesh Metha na Mratibu wa Diaspora
Zanzibar Hassan Hafidh.
Kushoto ya Balozi Seif
ni Afisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Makame Shauri, Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Sukari Viky Patel na Meneja Miradi wa Kiwanda cha Sukari
Tushar Metha.
Baadhi ya Wananchi,Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mhonda na watendaji wa Hospitali ya Jamii wakifuatilia maelezo mbali mbali yaliyokuwa yakitolewa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Hospitali hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa pamoja na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda akitembelea baadhi ya sehemu za kiwanda hicho.
Kulia yake ni Menaja Mradi wa Kiwanda Bwana Tushar Metha na kushoto yake ni Meneja wa Kiwanda Viky Patel.
Tushar Metha Meneja
Miradi aliyevaa koti akimpatia maelezo Balozi Seif harakati
zinazochukuliwa na kurekebisha baadhi ya mitambo ya kiwanda wakisubiri
uzalishaji baada ya kupea kwa miwa mashambani.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif : Wanadiaspora kuwekeza nyumbani ni mwanzo mzuri
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Kitendo cha Diaspora kuamua
kuwekeza Zanzibar ni mwanzo mzuri wa kuitikia wito wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar wa kuwataka Wazaliwa wa Zanzibar walioko nje ya
nchi kuanzisha miradi ya kijamii nyumbani kwao.
Balozi Seif alitoa
kauli hiyo wakati wa hafla maalum ya kuzindua Hospitali ya Jamii
inayosimamiwa kwa pamoja kati ya Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda
wakishirikiana na Vijana wa Diaspora wenye asili ya Zanzibar hapo
pembezoni mwa majengo ya Kiwanda cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Alisema hatua ya
wawekezaji hao walioamua kuanzisha miradi ya kijamii katika sekta ya
afya umekuwa wakati muwafaka kwa vile unakwenda sambamba na azma ya
Serikali Kuu ya kuimarisha sekta ya afya nchini.Balozi Seif alisema
hospitali hiyo itakayokuwa ikitoa huduma za matibabu mbali mbali kwa
mchango mdogo itasaidia wafanyakazi wa kiwanda cha sukari Mahonda
sambamba na Wananchi walipo pembezoni mwa kiwanda hicho.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kuyakaribisha na kuyatia moyo makundi ya Diaspora ili yaendelee kuwekeza
katika miradi tofauti kwa lengo la kusaidia ndugu,jamaa na wazazi wao.
“ Mchango wa Kiwanda
cha Sukari kilichoshirikiana na Diaspora hao kimeisaidia Serikali katika
sera zake za kuwa na kituo cha afya kila baada ya kilomita tano hapa
nchini “. Alisema Balozi Seif.
Aliwakumbusha na
kuwanasihi wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao kwa kuitumia
hospitali hiyo yenye huduma na wataalamu waliobobea katika kufahamu afya
zao.
Balozi Seif alisema si
vyema kwa watu kusubiri maradhi yakajichomoza wakati ambao inakuwa
vigumu kwa madaktari na wataalamu wa afya kuyatibu maradhi hayo.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kiwanda cha sukari Mahonda kwa
ustahamilivu wake mkubwa kutokana na changamoto nyingi walizopambana
nazo hasa suala gumu la mashamba ya miwa ambalo lilikuwa likivamiwa mara
kwa mara na mifugo pamoja na baadhi ya wakulima.
Alisema
changamoto hizo zilizikuwa zikisababishwa kwa makusudi na baadhi ya
wanasiasa kwa lengo la kujijengea ngome za kupata kuungwa mkono na
wananchi hasa wakulima hao wakati wa changuzi mbali mbali.
Alieleza kwamba
Serikali kupitia watendaji wake ilikuwa ikichukuwa juhudi za kutafuta
ufumbuzi wa tatizo hilo kwa njia za mazungumzo hagtua ambayo inaonekana
kufanikiwa kwa kiwango kikubwa hivi sasa.
Hata hivyo Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatanabahisha wananchi hasa wakulima wa
pembezoni mwa mashamba ya miwa kwamba hatua waliyokuwa wakiichukuwa
kulima mpunga na viazi katika mashamba ya miwa ilikuwa ni makosa.
Alisema Serikali
iliamuwa kukaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuwekeza
miradi yao ambao kwa asilimia kubwa husaidia kutoa ajira kwa wananchi
sambamba na kuongeza mapato ya Serikali.
Mapema Mwenyekiti wa
Diaspora ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Jamii Mahonda
Dr. Ameesh Metha alisema huduma zitakazotolewa kwenye Hospitali hiyo
zitamuwezesha hata mwananchi wa kawaida kumudu kuchangia.
Dr. Metha alisema
Hospitali hiyo itakayohudumia Wafanyakazi wa kiwanda pamoja na wancnhi
wa vijiji vya jirani inaanzia na huduma za Xray, Uchunguzi wa Tumbo
{Utra sound }, dawa za maradhi mbali mbali na maabara.
Alisema huduma
nyengine muhimu kama uchunguzi wa figo,huduma za Meno, Macho na mazoezi
ya viungo zinatarajiwa kutolewa baada ya miezi sita kuanzia sasa.
Mganga Mkuu huyo wa
Hospitali ya Jamii Mahonda alifahamisha kwamba Uongozi wa Hospitali
umejipanga kufunguwa huduma za matibabu mbali mbali katika Vijiji vya
Nungwi na Kiwengwa miezi michache ijayo.
Dr. Amesh Metha
amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.
Ali Mohamed Shein kwa busara zake za kufikiria kuanzisha Diaspora hapa
Zanzibar.
Alisema uamuzi huo
umesaidia kutoa fursa, changamoto na ushawishi kwa Wazanzibari na
Watanzania walioko nje ya nchi kuhamasika na kushawishika kutaka
kuwekeza nyumbani kwao hapa nchini.
Chanzo: ZanziNews





No comments :
Post a Comment