dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 19, 2016

Askofu ataka Watanzania kuiombea Zanzibar

Rais Dk. Magufuli
Waumini wa dini na Watanzania kwa ujumla, wametakiwa kuiombea  Zanzibar ili iendelee na amani na utulivu kutokana na kukabiliwa na mvutano wa kisiasa.
 
Mvutano huo unatokna na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana na kuamuru urudiwe Machi, mwaka huu.
 
Wito huo ulitolewa juzi na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Juda Thadeus Ruwa’ichi, katika sherehe za kumsimika Askofu wa kanisa hilo, Jimbo la Mtwara, Titus Mdowe.
 
Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi na waumini wa Kikristo kutoka sehemu mbalimbali nchini.“Mnaweza kusema bara tumeshafanya uchaguzi wa Rais na ameshapatikana na maisha yanaendelea. Lakini haiwezi kuwepo ndoa ambapo mmoja wa wanandoa ni mgonjwa mkasema kwamba sisi tuko sawa. Ninawaomba Watanzania wote tuiombee nchi yetu, tudumishe umoja, upendo na amani ya taifa hili kama familia ya Mungu, alisema.
 
Askofu Mkuu Ruwa’ichi aliongeza kuwa: “Nawaomba na kuwaasa wote wenye uwezo wachangie kupatia ufumbuzi wa kufaa suala hili.  Tusifurahie wenzetu kuendelea kuvutana, kutishiana kuuana.  Hilo si jema, Zanzibar pakiwaka na Bara hapatokuwa shwari.”
.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughuliki Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Jenista Mhagama, aliwataka waumini wa dini kuendelea kuliombea dua taifa la Tanzania chini ya Rais Dk. John  Magufuli, ili liendelee kuwa la amani na utulivu.
Alisema suala la kulinda na kudumisha amani ya nchi ni la kila mmoja na kwamba viongozi wa dini watumie nguvu waliyo nayo ya ushawishi kuhubiri amani na upendo ili kuzidi kuijengea heshima nchi.
 
Alisema, Rais Dk. Magufuli amejipanga na amedhamiria kuleta mapinduzi ya kimaendeleo na zaidi kupambana na mafisadi na wavunjaji wa maadili kwa vitendo, hivyo anahitaji msaada wa maombi  kutoka kwa waumini wa dini zote kufanikisha azma yake hiyo.
 
Askofu Mdoe, aliyechukua nafasi ya Askofu Gabriel Mmole aliyestaafu baada ya kuitumikia kwa miaka 31, alisema atafanya kazi na watu wote bila ubaguzi na atamheshimu kila mtu.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment