dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 19, 2016

Kimbunga cha Rais Magufuli chazoa wakurugenzi wawili.

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.
Wakurugenzi wawili wa Manispaa za Kigoma na Mpanda mkoani Katavi, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo ubadhirifu wa zaidi ya Sh. milioni 300.
 
Hatua hiyo ya kuwasimamisha imechukuliwa na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.
 
Waliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma, Mhandisi Boniface Nyambele na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Suleiman Lukanga.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais (Tamisemi), Rebecca Kwandu, wakurugenzi hao wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuridhia na kutekeleza maamuzi ambayo yameisababishia serikali kupata hasara ya kiasi hicho cha fedha.Kwandu alifafanua kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Mhandisi Nyambele, anakabiliwa na tuhuma za uuzaji wa nyumba za Halmashauri bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo na bila kupewa kibali cha Waziri mwenye dhamana kama sheria inavyoelekeza.
 
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Lukanga wa Manispaa ya Mpanda, alisema anakabiliwa na tuhuma za ununuzi  wa gari hewa la kusomba taka kwa thamani ya Sh. 92,750,000 na ubadhirifu wa Sh. milioni 294 za ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Kakese.
 
Kufuatia tuhuma hizo, Waziri Simbachawene amemteua Mkuu wa Idara ya Maji,  Mhandisi Sultan Ndilowa, kukaimu nafasi ya Nyambele huku Akimteua Katibu Tawala Msaidizi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Lauteri Kaoni, kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda.
 
"Hatua inayofuata baada ya kusimamishwa kwa wakurugenzi hawa ni serikali kufanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo na watakapobainika kuhusika, mamlaka husika itachukua hatua," alisema Kwandu.
 
Simbachawene aliwataka wakurugenzi watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa kote nchini, kuwa waangalifu katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
 
"Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote watakaokiuka matakwa ya sheria, kanuni na taratibu kwa kuweka maslahi yao mbele," alisema Kwandu.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment