dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, June 27, 2017

JPM aagiza Watu hawa wakamatwe na wawekwe gerezani!

Pwani. Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, kuwanyang’anya viwanda wamiliki ambao wameshindwa kuviendeleza.

Ameyazungumza hayo leo (Alhamisi) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.

“Kipindi cha nyuma tulipofanya makosa ni pale tulipouza viwanda kwa watu binafsi, sasa  kuna  viwanda 197 vimeshakufa waliouziwa hawajishughulishi na vingine vipo kama magofu,” amesema.

Kutokana na hilo, Rais amesema; "natoa wito kwa wote waliouziwa viwanda kipindi cha nyuma na sasa wameshindwa kuviendeleza , naagiza sasa basi mrudishe  na wewe Waziri Mwijage tumia hata nguvu kama kuwaweka ndani weka tu siku akitoka huko atakuta kiwanda kimeanza kazi."

No comments :

Post a Comment