dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, June 30, 2017

Miswada 3 ya madini yatua Bungeni!

IKIWA ni siku kadhaa zimepita baada ya Rais John Magufuli kulitaka Bunge lipitie upya sheria na mikataba ya madini, miswada mitatu inayohusu madini tayari imesomwa bungeni kwa mara ya kwanza jana.

Aidha, ili kutoa fursa ya wabunge kujadili miswada hiyo iliyowasilishwa bungeni kwa hati ya dharura, vikao vya Bunge la Bajeti vilivyokuwa vifikie tamati leo, vimesogezwa hadi Julai 5 mwaka huu ili kutoa fursa kwa wabunge kupitia miswada hiyo. Miswada iliyosomwa kwa mara ya kwanza bungeni hapo ni Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.Muswada huu unapendekeza kuweka utaratibu ambapo wananchi kupitia chombo chao cha uwakilishi ambacho ni Bunge, kitapitia na kujadili makubaliano na mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi, ambayo imefungamana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujiridhisha na masharti. Muswada mwingine ni Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya nchi Kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017.

Muswada huu unakusudia kuweka masharti yatakayohakikisha kwamba hatua yoyote inayochukuliwa kuhusu uwekezaji wa rasilimali za taifa, inatambua na kuzingatia haki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama taifa huru lenye mamlaka ya kusimamia na kutumia rasilimali zake kwa maslahi ya taifa. Muswada mwingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017.

Wakati anapokea ripoti ya pili ya Kamati Maalumu ya Uchumi na Sheria kuhusu Taarifa ya Makinikia, Rais Magufuli aliliomba Bunge kupitia upya sheria na mikataba yote ya madini na gesi ili kuiepusha nchi kuingia katika mikataba mibovu.

“Kamati ya uongozi ilikaa jana (juzi) kubadilisha ratiba ambapo sasa mkutano huo wa Bunge la bajeti utaahirishwa Julai 5 mwaka huu, badala ya Juni 30 kama ilivyokuwa imepangwa awali, miswada mitatu mipya ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza, itapelekwa katika kamati za Bunge,” alisema Spika Job Ndugai, ili kutoa nafasi kwa wabunge kujadili miswada hiyo, Bunge limebadili ratiba kwa Bunge kuendelea na shughuli zake hadi Julai 5 mwaka huu, ambapo bunge hilo litaahirishwa.

Alisema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2017 kwa kuangalia upungufu uliojitokeza itafanyiwa kazi na Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohammed Mchengerwa.

Ndugai alisema pia Bunge limeunda kamati maalumu itakayoundwa na wajumbe wa kamati nne za Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Kamati ya sheria Ndogondogo na Kamati ya Katiba na Sheria, itakayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dotto Biseko ambayo itapitia miswada miwili ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017.

Pia kamati hiyo itafanyia kazi Muswada wa Sheria ya Mamalaka ya nchi kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017. “Kamati hizo zitafanya kazi kuanzia leo (jana) kwa kukutana na wadau mbalimbali na kisha taarifa itawasilishwa bungeni Jumanne, kabla ya bunge kuahirishwa Jumatano (Julai 5 mwaka huu),” Baada ya kuwasilishwa kwa miswada hiyo, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliomba mwongozo wa Spika, ambapo aliliomba bunge kuondoa hati ya dharura ya kujadili miswada hiyo.

“Muda mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa haraka haraka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo, “Kazi ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kwa umuhimu wake na maslahi kwa wananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, hivyo ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na hati ya dharura ikaondolewa na kuletwa bunge lijalo.

Aliongeza: “Kwa maelezo uliyotoa wadau wataitwa kwa short notice wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichambue. Huu ni mtego kwa kutufanya tushindwe kuishauri serikali kwa kazi yetu ya kibunge”. Akitoa majibu ya serikali kuhusu muongozo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulamavu, Jenista Mhagama alisema masharti ya kutunga sheria na masharti ya jumla, yamewekwa katika fasihi ya nane ya Kanuni za Bunge, masharti yameongezwa na kanuni ya 80 na kanuni nyingine.

“ Muswada ambayo imeletwa imekuja kwa hati ya dharura, ili bunge liridhie kama miswada hii inastahili kujadiliwa na bunge ama la, kanuni 80(4) inasema muswada wowote wa dharura hautaingizwa katika shughuli za Bunge bila kuwa na hati iliyowekwa sahihi na rais kuthibitisha kwamba muswada huo ni wa dharura. “Sisi kama serikali tumeshatimiza masharti yote, tumeshakamilisha hatua zote za kufikishwa muswada huo kwa hati ya dharura. Wanaoweza kulishauri Bunge baada ya kuona uzito wa kazi iliyolewa na serikali ni kamati husika itakayopewa kazi ya kujadili miswada hiyo,” alisema.

Alisema sio busara kwa wabunge kabla hawajaona yaliyomo katika miswada husika, kujenga hoja ya kuikataa ndani ya bunge, mana kinachofanyika ni kwa maslahi mapata ya taifa. Akijibu mwongozo huo, Spika Job Ndugai alisema kwa niaba ya wabunge alipokea hati ya dharura huku akiwataka wabunge kulifanyia kazi jambo hilo.

“Tulijadiliana na kamati ya uongozi yenye uwakilishi wa tukakubaliana suala hili lisonge mbele. Wakati Rais (Magufuli) akipokea ripoti ya pili ya mainikia, kwa niaba yenu nilikubali kama kuna mambo yenye maslahi kwa nchi tutayafanyia kazi, mambo yameletwa katika kamati husika, kamati itajadili kama muswada inastahili kuingia bungeni ama la hoja nitatokea huko.

Aliongeza, “kwa muda mrefu tulikuwa tunataka Bunge kuwa na nafasi fulani katika masuala ya yanayohusu maadini na gesi, liwe na nafasi fulani ili kuzuia nchi kuingia katika mikataba mibovu. “Miswada hii kama mtanzania yeyote mwenye kuhitaji ataipaata katika tovuti,”alisema Ndugai.

No comments :

Post a Comment