RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza matumaini yake makubwa kwa kuundwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) na kuanza kazi zake vyema tena kwa muda mfupi na kueleza kuwa kazi za Mamlaka hiyo zitaenda vizuri iwapo wataenda sambamba na sheria ya Mamlaka hiyo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Nd,Hassan Ali Mbarouk akitoa maelezo wakati wa kikao cha siku moja cha Ungozi wa Shirika hilo na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika kikao cha kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) pampoja na Uongozi wa ZECO katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 03/07/2017.
No comments :
Post a Comment