Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetapeliwa mamilioni ya fedha baada ya baadhi ya wafanyabishara wa mchanga kuwasilisha risiti za malipo hewa zinazoonyesha fedha zimelipwa benki.
Akizungumza na wandisihi wa habari katika idara ya misitu ya Zanzibar Waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohamed amesema Wizara imegundua utapeli huo mkubwa ambapo baadhi ya wafanyabishara hao kwa kushirikiana na wafanyakazi wa benki ya Zanzibar wamekuwa wakipigiwa muhuri wa kuonyesha malipo yamefanyika na kufanikiwa kujipatia rasimali hiyo bila malipo.
Mhe Hamad Rashid ambaye ni Waziri kutoka Chama cha upinzani cha ADC ndani ya serikali ya Zanzibar amesema pia Wizara imegundua kuwepo udanganyifu ambao unaofanywa na wafanyakazi na wenye magari kupakia mchanga zaidi ya ule uliolipiwa na kusababisha ukosefu na upandaji wa bei ya rasilimali hiyo na tayari magari 49 yamekamatwa na Wizara inadai shilingi milioni 58 za faini huku mikakati mipya ikanza kuwekwa.
Hata hivyo baadhi ya watuhumiwa ambao walikuwa nje ya jengo la idara ya misitu wamekanusha kuwepo kwa udanganyifu huo wa kuchuja zaidi ya kiwango kilichukubaliwa na kudai wamekuwa wakilipa fedha za ziada ingawa Mwenyekiti wa jumuiya ya madereva na matajiri wa magari ya wauza mchanaga Msabaha Hassan Silima amekiri kuwepo kwa udanganyifu wa stakabadhi feki za benki.
Raslimali ya mchanga Zanzibar hivi sasa imekuwa ni malighafi hali kiswani Zanzibar ambapo gari la tani moja bei yake hufika hadi shilingi laki sita wakati serikali inauza kwa shilingi 27,000 huku serikali imelazimika kupiga marufuku uuzaji na biashara hiyo sasa inafanywa na serikali.
No comments :
Post a Comment