Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Sunday, July 2, 2017

ZENJI YAPANGA KUANDAA MKUTANO MKUU WA DIASPORA!

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Ikulu), Issa Haji Ussi ‘Gavu’ amesema wanapanga kuandaa tena mkutano mkuu wa Watanzania waishio ughaibuni mwaka huu.

Gavu amesema tayari timu ya wataalamu imeanza kukutana kupanga eneo utakapofanyikia mkutano huo, mada zitakazowasilishwa pamoja na mambo mengi ambayo yanakwenda sambamba na malengo ya mkutano huo.

“Kamati ya wataalamu imeanza kukutana kwa kupanga utaratibu wote pamoja na idadi halisi ya washiriki, lengo kuu la mkutano huo ni kuwapa fursa Watanzania waishi nje ya nchi wakitoa michango yao ya kimawazo na maendeleo ili kuona ushirikiano kati yao na nchi yao unaimarika zaidi,” amesema.Amesema Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanao mchango mkubwa wa mawazo na kiuchumi ambao ukiwekezwa hapa nchini utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa.

Gavu amesema, licha ya mkutano huo, Zanzibar inajivunia kufanikiwa kutembelewa na watalii wengi mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita na kwamba, hali hiyo inaonyesha namna gani amani na utulivu vilivyotawala.
/ Mwananchi

No comments :

Post a Comment