Mbunge viti maalumu mkoa wa Kigoma Josephine Ngezabuke (CCM) amepata ajali mbaya ya gari akitokea Kakonko katika kijiji cha Mvugwe wilayani kasulu mkoani Kigoma Jana majira ya saa kimu na moja jioni.
Mbunge huyo amelazwa katika hospital ya wilaya ya kasulu, inaelezwa kuwa atakuwa ameathirika zaidi Mgongoni na kwamba hawezi hata kukaa.
Hata hivyo kesho Ofisi ya bunge inamtumia ndege maalumu kwaajili kumsafirisha Hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
No comments :
Post a Comment