dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 10, 2018

POLENI NDUGU ZETU WABARA!!!..........WATUMIAJI WHATSAPP BARA PIA WAANDIKISHWE NA WALIPISHWE!!!

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY

ISO 9001:2015 CERTIFIED
 
 





TAARIFA KWA UMMA

USAJILI WA WATOA HUDUMA ZA MAUDHUI KWA NJIA YA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaukumbusha umma kuwa, usajili wa watoa huduma za maudhui mtandaoni yaani wamiliki wote wa blogu, majukwaa mtandaoni (online forums), redio na televisheni mtandaoni ulioanza rasmi tarehe 21 Aprili, 2018 unaendelea na hadi tarehe 10 Juni, 2018 jumla ya leseni 46 zimetolewa na jumla ya leseni 4 zimekamilika kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi kwa wahusika.
Kwa mujibu wa Kanuni 4 na ya 14 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018 (The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations, 2018), watu wote wanaotoa huduma za blogu, majukwaa mtandaoni (online forums), redio na televisheni mtandaoni, wanatakiwa kujisajili TCRA na kupatiwa leseni ili kutoa huduma hizo. Jinsi ya kusajili tembelea tovuti ya TCRA katika kiunganishi: www.tcra.go.tz, kipengele cha Online Contents Application System'. Kwa ufafanuzi au maelezo zaidi tumia barua pepe: onlinecontent@tcra.go.tz
Pamoja na jukumu la kuelimisha Umma kuhusu Kanuni hizo na kuwasajili watoa huduma, TCRA imepewa pia jukumu la kuchukua hatua kunapotokea ukiukaji wa Kanuni za Maudhui Mtandaoni za 2018, kwa lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwa na matumizi sahihi na salama ya mitandao ya mawasiliano ya kielektroniki nchini.
Kwa hiyo, TCRA inaendelea kuutahadharisha umma kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 18 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za 2018, ni kosa la kisheria kutoa huduma za maudhui mtandaoni (blogu, majukwaa mtandaoni-online forums, redio na televisheni mtandaoni) bila kuwa na leseni.
MAMBO YA KUZINGATIA:
1.0        Wale ambao wamekuwa wakitoa huduma za maudhui mtandaoni na bado hawajapata leseni husika, wanatakiwa kujisajili kabla ya tarehe 15 Juni, 2018.
2.0        Kuanzia leo tarehe 11 Juni, 2018 hadi tarehe 15 Juni, 2018 hawaruhusiwi kuweka jambo/taarifa (post) yoyote zaidi ya zilizopo kwenye Blogu/Majukwaa/Redio auTelevisheni mtandao zao leo na ambazo zinapitiwa pia.
3.0        Baada ya tarehe 15 Juni, 2018 hatua za kisheria zitaanza kuchukuliwa dhidi ya yeyote atakayekuwa anatoa huduma za maudhui mtanadoni bila kusajiliwa na kupewa leseni kwa mujibu wa sheria.
  
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
11 JUNI, 2018


No comments :

Post a Comment