dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 8, 2018

Nchemba afunguka kwa mara ya kwanza tangu atumbuliwe!

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba mkoani Singida Dkt. Mwigulu Nchemba amejitokeza kwa mara ya kwanza hadharani jimboni kwake tangu asimamishwe kazi na Rais Magufuli.Mwigulu kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema amefanya mkutano na wananchi wa jimbo lake na kumshukuru Rais Magufuli kwa kumpumzisha kwani uongozi ni kupokezana.

“Nimefanya mkutano na wananchi jimboni Iramba, kushukuru chama changu CCM na Mh. Rais kwa nafasi aliyonipa ya utumishi.Uongozi ni kupokezana kijiti. Nawashukuru pia Wanairamba kwa mkutano mzuri,Sasa nitakuwa na muda mwingi zaidi wa kufuatilia miradi ya maendeleo ya jimbo langu hususani utekelezaji wa ilani ya CCM na shughuli mbalimbali za serikali.“ameandika Mwigulu Mchemba.

Mwigulu Nchemba alitenguliwa nafasi ya uwaziri na Rais Magufuli wiki iliyopita

No comments :

Post a Comment