dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 8, 2018

OMAN KUKIIMARISHA KIWANJA CHA NDEGE CHA ZANZIBAR!

NaThabit Madai, Zanzibar.

SERIKALI ya Omani imesema ipo tayari kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar ili ufikie vigezo sahihi vinavyohitajika kimataifa.

Imesema hatua hiyo inalengo la kuinua Zanzibar na kuwa na uwanja wenye ubora wa kimataifa kama uwanja uliopo Muscut, Omani.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Viwanja vya Ndege vya Omani Sheikh Aimen Ahmed Al-Hosni wakati alipofika na kufanya Mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Ofisini kwake Vuga Mjini Magharib Unguja.

Sheikh Aimen Ahmed Al –Hosni Alisema Serikali ya Oman tayari imeshajitolea kuisaidia Zanzibar katika hatua za ujenzi wa Uwanja huo kwa kadri ya mahitaji halisi yaliyopo ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano na uhusiano wa kidamu unaowaunganisha Wananchi wa Mataifa hayo Mawili.


Alieleza kuwa Uongozi wa Viwanja hivyo uko tayari kutoa mualiko kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Zanzibar kwenda kujifunza hatua iliyofikiwa kwenye uwanja huo wa Kimataifa.

Aidha Sheikh Aimen Ahmed alimthibitishia Balozi Seif kwamba ukweli ulio wazi ni kwa Wananchi wa Oman na Zanzibar kuona fahari wanapoendelea kushirikiana zaidi katika masuala ya Maendeleo ya Kiuchumi badala ya yale yaliyozoelekea ya Mila na Utamaduni unaofanana.

Naye Makamu wa Rais wa Viwanja vya Ndege vya Oman Bwana Ali Zaid alisema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat Nchini Oman hivi sasa umefikia nafasi ya 20 ya ubora wa huduma za Usafiri wa Anga Duniani kasi iliyotokana na Serikali ya Nchi hiyo kufanya juhudi ya ziada ya kuimarisha Miundombinu yake.

Bwana Zaid alisema Uwanja huo ambao kwa sasa unaongoza katika Ukanda wa Mataifa ya Mashariki ya Kati kwa kutoka huduma bora za viunganishi wa usafiri wa Anga pamoja na mambo mengine kwa Abiria ambapo pia tayari umeshatoa ajira zaidi ya Wafanyakazi 1,224.

Alisema wakati huduma za usafiri katika viwanja vilivyopo imeimarika zaidi malengo yametayarishwa kwa ujenzi wa Viwanja vipya Viwili katika Miji ya Muscat na Salala ili kuifanya Nchi hiyo ya Mashariki ya kati kuwa kiunganishi cha Usafiri kwa Bara la Asia na Bahari ya Pacific.




Makamu wa Rais huyo wa Viwanja vya Ndege vya Oman alisisitiza kwamba Oman kwa sasa imekuwa Mwanachama mzoefu katika utoaji wa huduma za usafiri wa Anga na kupata Tunzo kwenye Shirika la usafiri wa Anga la Kimataifa.

Akigusia masuala mengine ya Uchumi na Maendeleo Mmoja miongoni mwaWajumbe wa Msafara huo Bwana Mohamed Al – Mandhari alisema upo uwezekano wa Taasisi za Kiuchumi za Oman kuangalia uwezekano wa kuwekeza Miradi ya pamoja katika Sekta ya Umeme na Kilimo.

Bwana Mohamed alisema Taasisi hizo zina uwezo wa kuzalisha Umeme Megawati 30 kwa wakati mmoja zinazoweza kusaidia huduma za wazalishaji wadogo wadogo sambamba na Kilimo cha kisasa kinachoweza kutoa ajira hasa kwa Wajasiri Amali.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar bado inaendelea kutumia njia moja ya Umeme katika matumizi ya Taasisi za Umma pamoja na Wananchi jambo ambalo ni changamoto inapotokea hitilafu.

Alisema uwezo wa Mradi huo wa Umeme unaotegemea nguvu za jua unaweza kuwa mkombozi hatua itakayoweza kuongeza kasi ya ushirikiano uliopo baina ya Zanzibar na Oman zenye mafungamano kwa karne nyingi zilizopita.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi huo wa Viwanja vya Ndege vya Oman kwenye sekta ya Umeme una fursa ya kuandaa utaratibu wa kuandika Maombi yatakayowasilishwa Serikalini kwa hatua zinazofaa.

Alisema Zanzibar kwa muda mrefu tayari imeshajipanga katika uimarishaji wa Uchumi wake kwa kujenga miundombinu kwenye sekta tofauti ili kujiweka tayari kuingia katika mfumo wa uchumi wa Kati wa Viwanda.


No comments :

Post a Comment