Dr. Anita Coordinator, Adult ESOL and Basic Skills for College and Careers ikiwemo workforce Development and Continuing Education akitoa somo kwa wanawake DMV waliojitokeza kuhudhuria darasa elekezi kuhusu fursa zilizopo ikiwemo elimu bure kwa wanawake ikiwemo ya chuo kikuu kwa wanawake wanaolea watoto peke yao. Darasa hili lililofanyika siku ya Jumamosi Jan 19, 2019 katika chuo cha Montgomery liliratibiwa na Jumuiya ya waTanzania kwa kushirikiana na kamati ya wanawake na watoto DMV na khuhudhuriwa na wanawake 44 kutoka kila pembe ya DMV japo katika uandikishaji walifikia wanawake 66.
Wapili toka kushoto (waliokaa mbele) ni Joha Nyang'anyi Makamo wa Rais Jumuiya ya waTanzania DMV akiongoza wanawake wenzake DMV kwenye darasa hilo kushoto waliokaa mbele ni Mariam Mashaka na Kulia ni Gloria Alex first Lady mlezi wa kamati ya wanawake na watoto wakimsikiliza Dr. Anita Mwalui (hayupo pichani).
Dr. Anita Mwalui akitoa elimu elekezi kwa fursa za wanawake DMV katika chuo cha Montgomery kilichopo Kampasi ya Silver Spring /Takoma Park jimbo la Maryland.
Juu na chini ni wanawake waliohudhuria darasa hilo.
Picha ya pamoja. Kwa picha zaidi tembelea tovuti ya jumuiya ya watanzania DMV www.tanzaniancommunitydmv.org
No comments :
Post a Comment