Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, March 25, 2019

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Idai yaongezeka!


Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na kimbunga Idai kilichoikumba eneo la kusini mwa Afrika zaidi ya juma moja lililopita,imeongezeka kwa kasi siku ya Jumamosi.

Idadi ya waliothibitishwa kupoteza maisha nchini Msumbiji imeongezeka kutoka 242 mpaka 417,waziri wa ardhi na mazingira nchini humo Celso Correia ameeleza, Idadi hii mpya inafanya waliopoteza maisha Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kufikia 700, Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi.


Kimbunga kimeua takribani watu 259 nchini Zimbabwe na Malawi 56, Watu walipoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko.

Lakini Umoja wa mataifa umesema maafisa wataweza kutathimini madhara pale maji yatakapopungua.

Ofisi ya Umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinaadamu, OCHA imesema kuwa mto wa Buzi na Zambezi iko kwenye hatari ya kuvujika kingo zake kwa mara nyingine.

''Tutasubiri mpaka maji yaliyotokana na mafuriko yaishe kisha tutafahamu kwa hakika kuhusu idadi ya waliopoteza maisha nchini Msumbiji.Mratibu wa OCHA Sebastian Rhodes Stampa alieleza.

Maelfu wamenasa kutokana na mafuriko, na vituo vingi vya uokoaji vya nchini Msumbuji vimeanza kupokea vyakula.

Watu takriban milioni 1.7 wameathirika kusini mwa Afrika, wakiwa hawana umeme, na maji hasa kwenye maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho.

No comments :

Post a Comment