dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 8, 2019

Mugabe kuzikwa katika makaburi ya mashujaa Zimbabwe!

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe atazikwa kwenye makaburi yalioko kwenye kilele cha kilima, ambayo yamehifadhiwa makhsusi kwa watawala wa Zimbabwe, amesema afisa wa serikali mnamo wakati taifa hilo la Kusini mwa Afrika likianza rasmi hii leo, siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa zamani.

Bado tarehe kamili ya maziko haijatangazwa na haijulikani ni lini mwili wa Robert Mugabe utarejeshwa nchini kutoka Singapore alikofariki wakati anapokea matibabu.
Mugabe aliyefariki akiwa na miaka 95 atazikwa katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa kulikotengwa kwa raia wa zimbabwe waliyochangia pakubwa wakati wa vita dhidi ya utawala wa wazungu wachache.

Baadhi ya wazimbabwe wanamuona Mugabe kama muafrika halisi na mkombozi na wengine wanamuona kama muovu aliyeletea mateso na uharibifu nchini humo.

No comments :

Post a Comment