dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 8, 2019

WATANZANIA WAICHAMBUA VITA VYA WENYEJI NA WAGENI KULE SOUTH AFRICA!

CHANZO CHA VITA VYA WENYEJI WA AFRIKA  KUSINI NA WAGENI NI SERA MBOVU YA ELIMU  AFRIKA KUSINI BAADA YA MKATABA WA UHURU YAANI FREEDOM CHARTER

Kuanzia Oktoba mpaka  Disemba 2015 nilikuwa mwanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Wits kilichoko katika  Jiji la Johannesburg katika Kitengo cha Global Labour University maarufu kama GLU. Nilirudi Tanzania kupiga kura na  baada YA kupiga kura nilirudi  Afrika  Kusini kuendelea na masomo yangu. Kabla  YA kwenda Afrika Kusini nilihudhuria mafunzo maalum Chuo Kikuu cha Shirika  la Kazi Duniani  Turin Itali na nilipomaliza masomo hayo Itali nilirudi nchini Ijumaa na Jumapili nikaunganisha kwenda Bondeni  kama wanavyoita vijana  wetu. 

Nikiwa  Afrika Kusini pamoja na kusoma mambo mengi kwa muda  huo swali kubwa  ambalo nilitaka majibu yake lilikuwa ni  kwanini vijana wa Afrika Kusini wanawabagua watu waliowakomboa. Swali hili lilitupwa  kwa Profesa  wetu wa Sosiolojia hapo Wits University lakini  tukaingia pia mitaani na sehemu  mbalimbali kusaka majibu kwa njia YA utafiti unaojulikana kama ethnographic method yaani  utafiti wa kufanya kwa kushiriki na kwa kuona  kinachoendelea.
Nilitembelea sehemu zote muhimu Johannesburg  na pembezoni ikiwa ni pamoja na magereza YA zamani  walikofungwa wapigania uhuru  na hasa  sehemu ilipotangazwa Mkataba  wa Uhuru maarufu kama Freedom Charter we nye vipengele zaidi  ya 10. Katika uchunguzi huo yafuatayo yalibainika:
1. Zaidi ya wafanyakazi milioni 3 kwenye migahawa na hotelini yaani hospitality industry wanatoka Zimbabwe kwa sababu Afrika Kusini hawana wazalendo wenye  ujuzi huo. Kwanini hawana? Vuta subira.
2. Asilimia 60 ya wafanyakazi kwenye mashamba ya Wazungu wanatoka nje ya Afrika Kusini kwanini?. Kwa sababu vijana wao  hawana ujuzi unaohitajika na pia bado  wanaona  ni utumwa kufanya Kazi kwenye mashamba ya Wazungu. 
3. Asilimia 60 ya watumishi kwenye Sekta  ya ujenzi wanatoka Msumbiji kwa kuwa  hawana wataalamu wa faini  hiyo wanaohitajika kuajiriwa.
4. Zaidi ya Asilimia 60 ya waajiriwa kwenye migodi wanatoka nje ya Afrika Kusini kwa sababu ya nchi  jirani zenye kuzalisha wafanyakazi na uchumi wa nchi hizo kuwa mbovu. 
5. Kazi nyingi Afrika Kusini zinahitaji ujuzi wa Diploma na Cheti kutoka kwenye vyuo visivyotoa shahada. Watoto wa Afrika Kusini hawapendi  kusoma kozi hizo na siyo Sera inayotiliwa mkazo na nchi.

Kwanini Afrika Kusini ilifikia hapo? Tulibaini sababu zifuatazo kuwa zimefikisha Afrika Kusini hapo ilipofikia.
1. Freedom Charter ilipinga ubaguzi na ukaandaliwa Sera ya waafrika  weusi wa Afrika Kusini kusoma katika vyuo vikuu vya  wazungu  hivyo  mlango  ukafunguliwa mtoto  kusoma katika Chuo Kikuu chochote.  
2. Freedom Charter haikufikiria kuwa ili nchi ikuze ajira, zaidi ya Asilimia 50 ya wahitimu wanapaswa kuwa na technical education yaani wakawa ni technicians wenye ujuzi ngazi ya Cheti na Diploma.
3. Technical and Vocational Education haikuwa  Sera iliyotiwa mkazo Afrika Kusini isipokuwa mkazo ulikuwa kwenye elimu  ya Chuo Kikuu na fedha nyingi zikaelekezwa huo na baada ya miaka 10 ya utekelezaji wa Freedom Charter, nchi ikajawa na wasomi wenye elimu ya vyuo vikuu huku Technical and Vocational Training ikiendelea kudharauliwa na kufifia hasa katika maeneo ya hospitality,  ujenzi na kilimo maeneo yenye ajira nyingi kwa wageni. 
4. Wazungu walipopanua ajira katika maeneo hayo, wakakosa wazalendo wenye ujuzi katika ngazi ya Certificate and Diploma. Wasomi wengi wakawa wa Shahada ambazo  hazikuhitajika kwenye soko la ajira. Njia pekee ilikuwa  ni kuajiri  wageni wenye ujuzi unaotakiwa.
5. Hatua hii ya Afrika Kusini kuzalisha wasomi wasiohitajika kwenye soko ndo  chanzo  cha wazawa kuwaona  wageni kuwa wanachukua ajira zao na kuanza  kuwachukia.
6. Mazingira ya makuzi ya watoto  Afrika Kusini yanachochea uhasama kwani  bado wanafundishwa kuwaona wazungu kuwa ni watu wabaya na wakandamizaji waliowaua  wazazi au mababu  zao. Elimu ya kuishi kwa Amani na adui haipo  Afrika Kusini. Lugha  ya mawasiliano nayo ni tatizo kwani wanaweza kubaguana kwa koo. Vile vile  sheria  zao bado ziko dhaifu sana. 
7. Niliambiwa japokuwa sikuithibitisha kuwa Freedom Charter utekelezaji wake katika Kipengele cha usawa wa kijinsia imesababisha matatizo makubwa Afrika Kusini kwani binti  akipata ujauzito akijifungua mlezi wa mtoto anapata  posho  ya kumlea mtoto wakati mama yake akiwa shule.  Utaratibu huu unawachochea wazazi kupenda watoto wao wazae halafu  wawatunzie watoto wakiwa shule kwani watapata posho. Sikulithibitisha kabisa suala hili.
8. Kimsingi  zaidi ya asilimia 60 ya Kazi zilizoko Afrika Kusini zinahitaji wahitimu wa elimu ngazi ya Cheti na Diploma yaani waliosomea Technical and Vocational Education wakati zaidi ya asilimia 60 ya vijana wa Afrika Kusini wana  Academic certificates katika ngazi  ya Shahada ambazo hazina  ajira.
9. Walioshikilia Ajira Afrika Kusini ni Wazungu hivyo wanaweza katika maeneo ambayo  wanaona kuna  usalama zaidi na pia wanapowaajiri wageni misuguano mingi  inapungua sehemu za Kazi. 


Kwa msingi  wa maelezo  hayo, mfumo wa elimu ndiyo imewaweka wahitimu wa Afrika Kusini mahali  walipo.  Wanaona nafasi zao za ajira zimechukuliwa na wageni wakati hawana sifa na ujuzi wa kufanya Kazi hizo hata  kama wageni wataondolewa. NI vigumu sana kwa Afrika Kusini kurudi kwenye reli  mpaka waingie kwenye Mtaala na Sera wapunguze wasomi wa vyuo vikuu wahimize elimu katika ngazi ya Technical and Vocational Education. Pia wawabadilishe mawazo watoto wao kuona Kazi kwenye kilimo, hospitality  industry  na ujenzi kuwa ni Kazi za watumwa walivyotumikishwa wazazi wao. Hilo linahitaji nchi kujipanga upya ila kwa sasa twende  na Kitabu  nikipendacho cha "Things fall Apart"

MTANZANIA WAPILI AELEZA:
Ngoja niwape kidogo story ya hapa South Africa. 
Ukifuatilia kiundani kuna ukweli kwanini Wazulu au raia wa mataifa mengine inaonekana wanabaguliwa na kuuwawa?

1.Sheria ya South Africa ya mauaji bado haijabadilishwa kutoka ile ya kaburu ya kwamba unaua mtu halafu unapelekwa Polisi wanakuja ndugu zako wakuwekea dhamana unarudi nyumbani unaendelea na kazi yako kesi inakwenda mahakamani sasa fikiria aliyekufa sio raia wa Nchi hii niambieni ni ndugu gani atoke labda Tanzania au Nigeria kuja kusimamia kesi?inasomwa mara 3 hakuna mlalamikaji basi inafutwa.

2.Hata sisi wageni tunatatizo kwa upande mwingine.Kwanza hawa watu tumewabadilisha utamaduni ambao hawakuwa nao mfano kuhonga mwanamke kwao ni kosa sasa sisi wageni tunahonga na hao wadada wanaanza kuwakataa kaka zao wanapenda wageni wao wanaita (Makwelekwele) na kaka zao nao hawakubali ukizubaa tu unapigwa bunduki tena nyumbani kwako.

3.Ukioa Mzulu inabidi usiwe na wivu kwani anaweza kuondoka nyumbani ijumaa akarudi j3 asubui na anakwambia kabisa alikua club?ukimpiga anakwenda kuwaita kaka zake wa kitaa wanakuja wanakupiga na wanachukua kila kitu ndani ndoa kwaheri haijalishi umezaa naye.

4.Serikali ya South Africa mtoto akizaliwa anaanza kulipwa ni kama laki na ishirini; 120,000 ya Tanzania mpaka afikishe miaka 18. Hapo Serekali inaachana naye na ndio wanaoleta vurugu kwani walizoea hela sasa kafikisha miaka 18 account yake inafungwa wanaingia mitaani.

5.Wanasiasa ni tatizo huyu Rais wa sasa kwenye Kampeni aliwaahidi kuwa akipata urais foreigners wote ambao wanafanya kazi ambazo wazawa wanaweza kufanya atawafukuza sasa hajawafukuza wananchi wanadai ahadi na hasemi chochote

6.Ndani ya South Africa kuna Majimbo ambayo Rais hana nguvu Mfano Kwazulu Natal kule Chief wao ndiye wanamskiliza akisema leo kavamieni maduka ya wageni na chukueni kila kitu ni mali yenu wanakwenda hilo nalo ni tatizo.

7.Wageni na sisi tuna tatizo hasa kuuza bangi na madawa ya kulevya vijana wengi sana hapa ni mateja na ndio vibaka wapiga watu risasi utakuta anapo kuomba hela cha kwanza mwangalie vizuri je hana cha moto?ukiona hana unamchunia tu ila jiridhishe kwanza au mpe tu hela ndogo tu kama buku tu ya Tz.

No comments :

Post a Comment