dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 6, 2020

MH.MAKONDA ANAPASWA AONYWE NA MAMLAKA YAKE YA UTEUZI KWA KUPOTOSHA UMMA!

Mheshimiwa Paul Makonda

Abdul Nondo

Kabla Marekani hali kuwa mbaya Rais Trump alikuwa na maneno ya kejeli juu ya ugonjwa huu ya COVID19 ,akiita Chinese Viruses(Virusi vya china) na hata akijisifu namna gani Marekani haiwezi kuathirika.

Leo hii Marekani ndio nchi ambayo ina hali mbaya kuanzia maambukizi hadi idadi ya vifo, hadi kufikia Jana tar 4/April/2020 , Maambukizi (Confirmed Cases ) Ilikuwa 300,000  na vifo Ilikuwa 8,100.

Mh.Makonda  anasema ugonjwa wenyewe wa Corona ni "mafua tuu",na akiuliza nani amekufa na Corona? ,na kushangaa kwanini watu wametulia majumbani.Kwa ufupi anachokifanya Makonda ni kile alichokikemea Mh.Zitto Kabwe alipotoa ushauri wake kwa Mh.Rais," Viongozi kuepuka kauli zinazo kinzana  na Wataalamu".


Makonda anashangaa watu kutokwenda kazini ,ikiwa kuna watu ofisi zao zimefungwa Hotel kadhaa zimefungwa,Vyuo vimefungwa,Shule zimefungwa ,Makampuni ya usafiri nje ya nchi imefungwa .Yeye anashangaa watu kutokwenda kazini. Alafu hapohapo Serikali wizara ya Afya inasema watu watulie nyumbani.Makonda kuita ugonjwa wa Korona ni " fua " tuu ni kupotosha umma.

Najua jeuri hii ya kuita ugonjwa huu ni "tu-mafua" ni kwa sababu ya sisi kuona tuna idadi ndogo ya walioambukizwa,jambo hili linatuvimbisha kichwa.Kwa kauli za Makonda ni wazi anatamani serikali iseme hakuna ugonjwa wa Korona nchini Tanzania hata kama upo , anatamani hata serikali idanganye kuhusu idadi ili ionekane idadi ipo ndogo .Shida yake apate kauli ya kusifu "Serikali ya Tanzania chini ya John Pombe Joseph Magufuli haina maambukizi",Kwake yeye anaona ndio njia ya kupata sifa.

Mh.Makonda amekashifu watu wanao hoji kuhusu idadi ya maambukizi,Makonda ameonesha kukasirika .Kana kwamba watu wanao hoji idadi , wanatamani idadi iwe kubwa, hapana sio hivyo .Ila hakuna uhalisia wa hali ya mazingira na takwimu au idadi.

Mfano,Nataka nitumie nchi ya Rwanda.

Rwanda ni nchi yenye Raia Mil.12.95  ,Wakati ugonjwa huu ukiwa umeshamiri nchini China huko Wuhan 2019 December,Rwanda iliunda "Multidisciplinary team"  timu ya Wataalamu tofauti kutathimini maandalizi ya kupambana na ugonjwa huo na namna ya kuzuia usiingie nchini Rwanda.

Moja ya njia kubwa waliyotumia ni kuweka screen kubwa inayochunguza "Fever au homa " ya abiria yeyote katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kigali.Na vifaa hivyo vilisambazwa maeneo mengine ya mipaka.

Kipindi hicho Tanzania tulikuwa tunaruhusu watu kuendelea kuingia bila kuchekiwa na hadi watu walishangaa mmoja wa mhudumu wa KIA uwanja wa ndege Kilimanjaro,alisema waziwazi "Idadi ya wachina wanaoingia kwetu wameongezeka".Hivyo  ni wazi Tanzania kuanza kuzuia na kupima watu mipakani na viwanja vya ndege tulichelewa kidogo.

Rwanda nchi yenye Raia Mil.12.95 ina idadi ya wagonjwa wa korona waliothibitishwa siku ya leo ni 102 , Tanzania nchi yenye raia zaidi ya milion 50 ina wagonjwa wa Korona 20 kwa taarifa za tar 3/April/2020.

Kenya ina wagonjwa 126,Uganda ni 48 . Tanzania ni 20 ,Je kwanini tuna namba ndogo ? 

Mbali na hatua nyingi zinazo chukuliwa na serikali kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu ,ila suala la kuwa na idadi ndogo ya wagonjwa wa korona sio kwamba nchi yetu ipo salama sana kushinda Rwanda ,au Uganda ,au Kenya Ila kwa tathimini za haraka Tanzania ndio nchi ambayo tulichelewa kwanza kuchukua hatua ,pili ndio nchi ambayo tahadhari zetu bado ni ndogo sana hatuna partial Lockdown ,wala hatuna total Lockdown kwasababu bado tunajiona hatuna maambukizi makubwa na tunaita ugonjwa huu ni "tu-mafua" .

Na hii ni kwasababu ya upimaji hafifu yaani upimaji wetu ni wa kusua ,sua tuu. Ndio maana ukisoma taarifa kutoka wizara ya Afya iliyotolewa na Waziri Ummy Mwalimu tar 3/April/ 2020 inataja No Confirmed Case ,hakuna maambukizi, wagonjwa ni 20,Kifo kimoja ,walioko katika Quarantine ni 130 .

Una jiuliza kama ,New Confirmed Case ni "0 " yaani hakuna mgonjwa mpya ,kwanini  hatuambiwi ni Zero (0) kati ya wangapi walio pimwa(tested) ? ,maana kama hupimi mtu ni wazi maambukizi mapywa utapata Zero (0 )tuu ,ukipima watatu  unaweza pia kutopata mwenye maambukizi mapya ,Ila ukipima wengi ndio njia ya kujua na kujitathimini tuna maambukizi mapya au hatuna .Je, serikali mbona haisemi idadi ya waliopimwa kama wanavyosema Kenya ,Rwanda na nchi zingine ?

Hatupaswi kujipa moyo wakati underground kuta hali ni mbaya ,tunapaswa kutoa idadi pia ya waliopimwa ili tukisema mgonjwa mpya 1 tujue ni kati ya wangapi waliopima ndio namna ya sisi wenyewe kujitathimini tupo katika hali gani.

Shukrani.


Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa,Act wazalendo.

Tar 5/April /2020.

No comments :

Post a Comment