dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 28, 2022

KESI YA WANA-DIASPORA KUPELEKWA MAHAKAMA YA AFRIKA!

  • AANDIKA MWENYEKITI WA MPITO WA TFDC  - "IKICHANGANYWA NA SIASA KESI TUTAWEZA KUIPELEKA MAHAKAMA YA EAST AFRIKA AU YA AFRIKA KUTAFUTA HUKUMU BORA ZA KISHERIA"!

Baada
ya kufahamika kuwa kundi la WhatsApp la Wana-Diaspora wanaojiita kama "TANZANIANS FOR DUAL CITIZENSHIP (TFDC)" kuonesha nia yao ya kuenda mahakamani, wengine walizuka wakiwalaumu kuwa wanataka kuishitaki serikali ya JMT. 

Blog hili baada ya uchunguzi limegunduwa kuwa hapakuwa na nia ya kuishitaki serikali bali kupata ufafanuzi wa masuala fulani fulani juu ya Katiba yetu ya JMT.

Aandika mmoja wao wa kundi la TFDC leo kuwa..." Nadhani kuna mahali kitu hakijaeleweka. Hakuna anayekuenda 'kupingana na serikali'.
Kinachofanyika, kimsingi, ni kuenda kupata ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na suala la Kikatiba (Constitutional Review) katika suala la uraia ikiwemo haki sawa kwa wanawake kwa wenza wao kupatiwa uraia, n.k", alimaliza mmoja wao huyo.

Mwengine wa TFDC alifafanuwa kwa kuandika..." 1) kesi yetu sio kesi dhidi ya serikali. Sisi tunapeleka kesi Mahakama Kuu ili watupatie tafsiri sahihi ya sheria ya uraia ya mwaka 1995".

Mwana-TFDC mmoja alitoa ushahidi wa provision moja kwenye sheria  ya uraia ya 1995 inayomruhusu mgeni kuchukuwa uraia wa Tanzania bila kupoteza uraia wa nchi yake. Provision hio aliitoa kwenye image ya hapa chini:
Mwenyekiti wa muda/mpito wa TFDC nae pia aliingia hewani kwa kuandika yafuatayo na huku akisisitiza kuwa hawaishitaki serikali bali wanataka ufafanuzi wa mambo fulani ndani ya Katiba ya JMT. Nae aliandika kuwa...

"1) Katiba ya Tanzania ya mwaka 77 hailezei kinagaubaga tafsiri ya uTanzania.

Haisemi MTanzania ni Nani?

Hili linapekea kuwepo na matatizo mengi ya watu kusingiziwa uraia wa nchi zingine", na hapa Mwenyekiti alitoa mfano wa watu wawili mashuhuri nchini waliosingiziwa kuwa hawakuwa raia.

Akaendelea Mwenyekiti huyo wa muda wa TFDC kwa kuandika kuwa...

"Kesi hii itaitaka mahakama kuitaka serikali iweke bayana kwenye katiba tafsiri sahihi ya uTanzania na marekebisho ya katiba juu ya Jambo hilo.

2) Ibara ya tano ya katiba ya JMT inaongelea haki ya kupiga kura. Kifungu cha pili cha ibara hiyo kinasema, nanukuu sio word for word—“Katiba inalipa Bunge la JMT kuweka zuio la kupiga kura kwa MTanzania mwenye uraia zaidi ya nchi moja.

Katiba haisemi kinagaubaga juu ya kulipa mamlaka Bunge la JMT kumfutia raia wa Tanzania uraia wake pale atakapo chukua uraia wa nchi nyingine.

Tutaiomba mahakama kutoa tafsiri sahihi ya kifungu hiki cha katiba.

2) Katiba ya Tanzania inazuia utengenezwaji wa sheria ndogo za kibaguzi. Everyone should be treated equally under the law. Lakini sheria ya uraia ya mwaka 1995 inawapa wanawake uraia pacha endapo wataolewa kwenye nchi zinazowapa wanawake hao uraia kwa kuolewa.

Hii ni sheria baguzi na hivyo kuifanya sheria ya uraia ya mwaka 1995 kuwa sheria batili.

3) Kukosekana kwa due process kwenye suala la uraia. Katiba ya Tanzania inasema mtu hawezi kupoteza uraia wake bila ya due process. Lakini, citizenship Act ya mwaka 1995 inamnyang’anya MTanzania uraia wake automatically. Hii sheria inakinzana na matakwa ya kikatiba.

4) Citizenship Act ya 1995 inabagua watu waliyoowa ama kuolewa na raia wa nchi nyingine kwa kuwapatia wanawake waliyoolewa na waTanzania wa kiume a pass to Citizenship na kuwanyima njia hiyo wanaume waliyoowa wanawake wa kiTanzania.

Sheria hii ina ubaguzi wa kijinsia kitu ambacho Katiba yetu hairuhusu.

Kuna vifungu vingi vya sheria ya uraia ya mwaka 1995 vinavyokinzana na sheria mama (Katiba)".

Mwenyekiti huyo wa muda aliimaliza msg yake kwenye group kwa kuandika waziwazi kuwa kama wakishindwa kesi yao kwasababu za kisiasa basi wataweza kuipeleka kwenye Mahakama ya East Afrika ama Mahakama ya Afrika kutafuta hukumu bora za kisheria.

Zanzibar Ni Kwetu (ZNK) imegunduwa kwamba wengine (sio wote) wanaoi-support Hadhi Maalum kwa nguvu zao zote ni kwasababu kama Tz  iki-adopt DC wao au wana-familia wao hawato-qualify. ZNK is sympathetic to them, lakini solution sio kutupiana matope.

For sometime, this will continue to be a grueling discussion online and a raucous one too, till our High Court comes out with a clear interpretation of our 1995 Citizenship Act!


CAUTION: Any opinion expressed in this blog does not necessarily reflect the view of the blog's owner.

No comments :

Post a Comment