Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZSSF

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Saturday, March 25, 2017

SIMBACHAWENE - WALIMU WALIOHAMISHWA KIUONEVU WALIPWE!

SERIKALI imetoa siku 30 kwa halmashauri nchini kuwalipa walimu wote waliohamishwa kwa uonevu na kupiga marufuku tabia ya kuhamisha walimu kwa kukomoana.
Pia walimu wakuu na wakuu wa shule waliokaa muda mrefu vituoni watahamishwa ndani ya miezi mitatu na uhamisho huo utafanywa na Wizara.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati akifungua mkutano mkuu wa maofisa elimu wa mikoa na wilaya.
Alisema walimu wote waliohamishwa kwa mtindo wa uonevu, wakuu wa shule wahakikishe wanalipwa fedha zao.
“Unamhamisha mtu bila kuwasiliana na Hazina. Mmekuwa kama kiwanda cha kuzalisha madeni ya serikali, halmashauri zinazalisha sana madeni mtalipa nini, kuhamisha mtu bila utaratibu ni kuongezea serikali madeni,” alisema.
Alisema kumekuwa na tabia ya kukomoana na maofisa elimu wanawake wamekuwa wanahamisha walimu wenzao bila kujali mazingira yake.

Jinsi Maulid Kitenge alivyomnusuru Nape na bastola!

MWANDISHI wa habari, Maulid Kitenge,  ambaye juzi alimnusuru aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye dhidi ya mtu aliyemshikia bastola wakati akielekea kuzungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Protea, jijini Dar es Salaam, amefunguka na kueleza kile kilichomsukuma aingilie kati.

Juzi, mara baada ya Nape kuwasili karibu na hoteli hiyo, ambayo inapakana na Kanisa la Mtakatifu Petro, lililoko eneo la Oysterbay, aliposhuka tu ghafla kijana huyo mrefu mweusi akiwa amevalia suruali ya jinzi, shati la mikono mirefu la mistari mistari pamoja na kofia, alimkimbilia na kumshika mkono kiongozi huyo akimtaka arudi kwenye gari.

Nape hakukubaliana na hatua hiyo, ambaye alimtaka kijana huyo aonyeshe kitambulisho, lakini hakufanya hivyo, zaidi alirudi hatua chache nyuma na kisha kutoa bastola iliyokuwa kiunoni kwake na kumtishia.

Wakati tukio hilo likitokea, ghafla alitokea kijana mwingine aliyekuwa amevalia suruali na fulana nyeusi akimsaidia yule aliyekuwa ameshika bastola kumsukuma Nape, ili arudi kwenye gari lake.


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yafanya ziara ya siku moja kisiwani Pemba!MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe:Omar Khamis Othaman, akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, wakati walipokuwa katika ziara ya siku moja kisiwani Pemba, kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

WAJUMBE wa kamati ya kudumu ya Bunge ya katiba na sheria, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe;Omar Khamis Othaman wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kufika ofisini kwake Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

MBUNGE wa Jimbo la Wingi Mhe:Juma Khamis Hamad, akichangia ripoti ya Tume ya haki za binaadamu na Mradi wa MIVARF, wakati wa ziara ya kutembelea miradi hiyo Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

Sababu za January Makamba kuamua kukaa kimya kwenye Mitandao ya kijamii!


Zanzibar ya adhimisha siku ya kifua kikuu duniani kwa kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu!

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma akifungua Kongamano la maazimisho ya siku ya Kifua kikuu Duniani katika ukumbi wa sanaa Rahaleo (kulia) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirman  na (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Taib.
 Mratibu kitengo cha ufuatiliaji na tathmini mwenendo wa maradhi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Ukoma Zanzibar Asha Ussi Khamis akitoa mada yake ya matokeo ya utafiti juu ya uelewa, tabia na matendo juu ya kifua kikuu Zanzibar katika ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.

 Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu walioshiriki Kongamano la maazimisho ya siku ya Kifua kikuu Duniani katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali alipokuwa akifungua Kongamano hilo.

CHADEMA WAFUNGUKA KUHUSU NAPE!

 Makamu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kuwateuwa Lawrence Masha na Ezekia Wenje kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki pamoja na mambo mbalimbali yayoendelea nchini. Kulia ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Demokrasia  na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais Dk. John Magufuli kuueleza umma wa Watanzania sababu za kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Katika hatua nyingine kimesema wabunge wa vyama pinzani kwa kushirikiana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi wanatarajia kuwasha moto katika Bunge la Bajeti linalo tarajia kuanza mapema mwezi ujao kulingana na mambo mbalimbali yautendaji wa Serikali ya awamu ya tano.

POLISI WAANZA KUMSAKA ALIYEMTOLEA BASTOLA NAPE!Jeshi la Polisi limesema limeanza kufanyia kazi maagizo waliyopatiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kumsaka mtu aliyemtolea bastola aliyekuwa Waziriri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Hayo yalisemwa jana na Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso. Awali, Mwananchililimtafuta Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu, lakini simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyemtaka mwandishi amtafute Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ili atoe ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa agizo la Waziri Nchemba.
Alipopigiwa simu, Senso alijibu kwa ufupi kuwa wameanza kufanyia kazi agizo la Waziri Nchemba.
“Sisi tumepokea maelezo ya waziri na tayari tumeanza kuyafanyia kazi, hilo ndilo ninaloweza kukwambia,” alisema.
Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya polisi aliyevalia kiraia kumtishia bastola, Nape ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM).