dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 12, 2012

CUF YASISITIZA ZANZIBAR KUWA NA MUUNGANO WA MKATABA

Zanzibar Minister for Constitution and Legal Affairs, Mr Abubakar Khamis Bakar

Written by ibnially  //  12/09/2012  
Na Masoud ali….

Mjumbe wa baraza kuu la CUF taifa ambae pia ni Waziri wa katiba na sheria ndugu Abuubakar Khamis Bakar amewasihi wananchi wa jimbo la Bububu kujitokeza kwa wingi kumchagua mgombea wa CUF ili kuongeza nguvu katika baraza la uwakilishi katika kulinda chama, jimbo pamoja na nchi. ili kuweza kuendeleza yale aliyaahidi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Bububu katika uwanja wa magengeni alipokua akiwahutubia wananchi pamoja na wapenzi wa chama hicho amesema kwa sasa Zanzibar haina uwezo wa kutoka kwenda nje ya nchi kutaka misaada bila ya kupitia Tanzania bara, ili kuondoa tatizo hilo na kuipatia Zanzibar mamlaka yake kamili ni lazima kuongezeka idadi ya wawakilishi wa CUF kupitia ISSA KHAMIS ISSA na kuepuka sera za CCM za kuwa na serikali mbili kuelekea serikali moja.


Amesema wakati umefika Zanzibar kuwa na Serikali yake, na Tanganyika kuwa na Serikali yake ili kupata muungano wa mkataba ili kukua kimaendeleo. hivyo amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwa na kauli moja katika utowaji wa maoni kuhusu katiba mpya.

Nae mgombea uwakilishi jimbo la Bububu amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpa ridhaa yao ili kupata Bububu mpya yenye maendeleo.

Ndugu ISSA KHAMIS ISSA amesema iwapo atachaguliwa na wananchi wa jimbo hilo ataimarisha sekta za maendeleo ikiwemo afya na michezo kwa vijana wa eneo hilo na kuhakikisha wanakuwa na timu yao itakayoshiriki ligi kuu zanzibar.

Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment