dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 23, 2012

Joseph Moses January Castico

Wasifu wa Marehemu Castico

Marehemu. Joseph Moses Castico

Sunday, September 23, 2012
Historia  fupi ya marehemu Joseph. Moses. January Castico.
 Marehemu Joseph Castico ni mtoto wa Sita katika Familia ya Mama Christina Mary Ali, na mtoto wa Kwanza wa Mzee Moses Joseph Castico.

Amezaliwa  tarehe 27-4-1952, katika hospitali ya Mnazi Mmoja, na kupata Elimu yake ya Msingi katika Skuli ya Convet Tumekuja na kuendelea na elimu yake ya msingi katika skuli ya St.PaulKiungani Unguja
Amepata elimu ya Sekondari katika skuli ya Lumumba kidatu cha Nne hadi cha sita.
Elimu ya Juu amepata katika Chuo cha Ualimu Bet-el-Ras Zanzibar na kuendelea na mafunzo ya Ualimu katika Chuo cha Ualimu Dar-es-Salaam na kupata shahada ya kwanza ya Ualimu.1975/1976

Marehemu Joseph Castico amepata mafunzo nje ya Nchi katika Nchi za Urusi,Sweden,Norway,India, Uarabun na kutembelea Mikoa ya Tanzania Bara kwa shughuli za Kikazi na Mafunzo.Alikuwa Mfanyakazi bora wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, na kufikia ngazi ya Ukurugenzi katika Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo. amepata tunzo mbalimbali wakati wa uhai wake na kuwa mfanyakazi bora mara mbili .

 Alikuwa mwanamichezo na Mwanamuziki na Mtungaji wa mashairi wakati wa uhai wake. Akiwa katika harakati za kuchapisha kitabu chake kinachosubiriwa kwa hamu na wasomi mbalimbali hapa Zanzibar kikiwa katika harakati za kuanza kuchapishwa kinachoitwa RAMCO.
Hadi mauti yanamkuta amekuwa na Cheo cha Msaidizi Mtendaji Kituo cha Kiswahili Ecrotanal Zanzibar, na Mwenyekiti wa ZIFF, Mjumbe wa BUSARA Zanzibar.
Marehemu amebarikiwa kupata Watoto watano na Wajukuu Wanne.ameacha Mke .
 Marehemu ameuguwa kwa mudu mfupi baada ya kuuguwa hafla shindikizo la Damu hadi kumkuta mauti tarehe 21-9-2012 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar juzi saa moja Usiku.


BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA MAPENZI YA BWANA YATIMIZWE.

XXX

Maziko ya Joseph Moses Castico Mwanakwerekwe Zanzibar.


 Askofu Mstaafu wa Kanisa la Mkunazini Zanzibar John Ramadhani, 
akiongoza Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu.

 Marehemu Joseph Moses Castico


 Waumini wa kanisa la Mkunazini wakiwa katika Ibada ya kuuombea mwili wa 
marehemu Joseph Castico, ikiongozwa na Askofu Mstaafu John Ramadhani.

 Mke wa marehemu Joseph Castico, Modline Castiko akiwa katika Ibada ya 
kuuombea mwili wa marehemu katika kanisa la Mkunazini Zanzibar.



 Father Masoud wa kanisa la Mkunazini akiuombea mwili wa marehemu 
wakati ukizikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe.

 Wananchi wakiupokea mwili wa marehemu Joseph Castico wakati ukizikwa 
katika makaburi ya mwanakwerekwe leo jioni.

 Mtoto wa pili wa marehemu akimliwaza mama yake wakati wa maziko ya baba yake.

 Waumini wa dini ya Kikristo na Wananchi wwengine wakiwa katika makaburi 
wakishuhudia mazishi ya Marehemu Joseph Moses Castico yaliofanyika katika 
makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.

 Mtoto wa kwanza wa Marehemu Lloyd Joseph Castico akiweka 
msalaba katika kaburi la baba yake baada ya kuzikwa katika 
makaburi ya Mwanakwerekwe.

 Mke wa Marehemu Moldine Castico akiweka shada la maua katika 
kaburi baada ya mwili wa marehemu kuzika katika makaburi ya 
Mwanakwerekwe Zanzibar.jioni ya leo na kuhudhuriwa na 
Wananchi mbalimbali.

Wananchi waliohudhuria mazishi ya Marehemu Joseph Moses Castico 
katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar jioni ya leo.

No comments :

Post a Comment