dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 14, 2012

Mifupa ya binadamu wa kale yapatikana Pangani

Archeology teams digging the past!


NA LULU GEORGE

Mifupa ya mtumwa wa kale inayokadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 1,700 imepatikana katika sehemu ya Kimu eneo la Bweni wilaya ya Pangani mkoani Tanga ikiwa bado imefungwa na minyororo katika mikono na miguu.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili jana, Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Historia na Akiolojia, Elinaza Mjema, alisema walikuta mifupa hiyo baada ya kuchimba ardhi wakiwa katika harakati za utafiti wa mambo ya kale.

Alisema eneo ambalo mifupa hiyo imepatikana ni lile lililokuwa likitumika kwa ajili ya kuvusha  watumwa kwenda zanzibar katika miaka ya 1,700 na 1,800.
“Eneo hili tulilokuta mifupa hii lilikuwa likitumika kwa ajili ya kuwavusha watumwa katika miaka hiyo ambayo biashara ya watumwa ilishamiri na huu ugunduzi tunaweza kusema ni wa kwanza kutokea katika Afrika Mashariki hivyo tuna kila sababu ya kujivunia,” alisema Mjema.

Alisema yeye kwa kushirikiana na wataalamu wengine kutoka UDSM wanatarajia kuchukua sampuli ya mifupa hiy na minyororo Novemba 17, mwaka huu ili kubaini umri wa mtumwa huyo, mwaka aliokufa na umri wa chuma kilichotumika kama minyororo.

Mjema alisema wanataka kubaini iwapo chuma hicho kilitengenezwa na Waafrika au Wazungu na kwamba kama ni Waafrika kitakuwa kimetengenezwa zaidi ya miaka 1,000 iliyopita.

Nao baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Pangani walisema ugunduzi huo utasaidia kuitangaza wilaya yao kwani ni kivutio cha pekee cha utalii na kutakuwa na ongezeko la wageni wa ndani na nje ya nchi watakaoongeza pato la wilaya.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment