dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 9, 2013

CCM Zanzibar kuanzisha saccos


Na Mwinyi Sadallah
9th March 2013

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewashauri Wawakilishi, Wabunge na Madiwani wake  kusimamia mchakato wa kuanzisha Saccos zitakazoyaunganisha makundi ya Wanawake na Vijana ili  kuzalisha ajira katika sekta binafsi.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, alisema wakati akifungua kikao cha watendaji wa CCM ngazi mbalimbali toka Mkoa wa Mjini na Magharibi kwenye Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja.
Mhandisi Masauni alisema kuna umuhimu wa kuitumia sekta binafsi ili kuongeza ajira zaidi kwa kuyajengea maarifa, uwezo na mbinu makundi ya vijana na wanawake chini ya mipango shirikishi jamii.
Akizungumzia kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2013/2014, Masauni alisema ipo haja na kwa viongozi kukaa pamoja, kutafakari na kupata njia itakayowafariji wanafunzi huku Serikali ikichukua hatua zaidi.
Amepongeza Serikali za chama chake kwa kuguswa na matokeo hayo na kuamua kuchukua hatua ya kulipatia ufumbuzi wa haraka suala hilo.
“Tumebahatika kuwa na viongozi wasikivu, jambo hili limewagusa, halikuwafurahisha, wamechukua hatua za haraka naamini mambo yatakwenda barabara na kupata tiba yake,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment